Baada ya CCM Kutimua Makada Wake 12 Waliokuwa Wanaimba Kuwa na Imani na Lowassa,Lowassa Aibuka na Kuwakaribisha Ukawa...!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.

Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.

Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.

Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.

Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.

Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.

Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.


Edward Lowassa

Mjumbe kamati Kuu Chadema
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanini hawajajiuzuru wenyewe mpaka wamefukuzwa kama kweri ni watu wazuri hata wewe mwenyewe wewe ulitaka kugombea kwa ticket ya ccm baada ya kukatwa ukahamia ukawa dariri mzuri ya kiongozi huonekana pale alipopewa madaraka tangia niko mdogo ulikuwa ccm lakini hata siku moja sijasikia umesidia watu au umeokoa pesa za serikali hamna M.h acha uchu wa madaraka kwanza ni mgonjwa hatutaki wanafiki na maselfish kama nyinyi pumzika kwa amani your days are numbered byebye see u at hell

    ReplyDelete
  2. Lowassa wewe uko chama Gani? Si CCM damu amu... Chadema tumeshalustukia.. Bado Kukawa.

    ReplyDelete
  3. HAPO NDIO CHADEMA TUNAKOSEA,HAKUNA HAJA YA KUWAITA WAJE ILA KAMA WANA MAPENZI NA CHADEMA WATAKUJA WENYEWE NA KABLA YA KUWAPOKEA WACHUJWE KWANZA.

    ReplyDelete

Top Post Ad