Fahamu Maajabu 41 ya Kazi ya Maji Mwilini Mwako..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Baadhi ya sababu kwanini unywe maji kila siku:

Je unazijuwa kazi za maji mwilini? Au ukishakunywa tu na kiu kukatika basi unakuwa huelewi nini kinaendelea baada ya hapo. Mashuleni umhimu wa maji mwilini unafundishwa kwa kiasi kidogo sana na mara nyingi maji ya kunywa yamefundishwa au kuchukuliwa kuwa ni kitu cha kusafirishia viini lishe toka sehemu moja au nyingine tu.

Lakini maji yana umhimu mkubwa mwilini zaidi ya hapo.

Tunaposema maji ni uhai huenda unaichukulia kauli hii kirahisirahisi tu, lakini leo utajuwa ni kwanini maji yaliitwa ni uhai. Endelea kusoma.

Baada ya oksijeni, maji ndicho kitu pekee ili kuishi. Zifuatazo ni baadhi ya KAZI 41 mhimu ZAIDI za maji mwilini:

1. Bila maji hakuna kinachoishi. Wakati wowote unapopungukiwa maji, baadhi ya seli zako ndani ya mwili hufa.

2. Panapotokea upungufu wa maji, kitu kimoja lazima kipotee, baadhi ya kazi za seli hufa.

3. Maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu, maji ndiyo hela ya mwili, bila kunywa maji ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

4. Maji hutumika kama moja ya malighafi katika usanifu na ujenzi wa seli, huziweka seli pamoja.

5. Maji hukinga uharibifu wa vinasaba (DNA), Vinasaba vichache visivyo vya kawaida huzarishwa.

6. Maji kwa uwezo mkubwa yanaongeza uwezo, nguvu na kinga ya mwili, ujuzi huu wote unahusisha pia dhidi ya kansa.

7. Maji ni wakala mhimu katika mmeng’enyo wa vyakula karibu vyote, vitamini na madini.

8. Maji yanatumika kusafirisha vitu vyote mwilini, maji yanapoifikia seli, huipa pia oksijeni na kuchukuwa hewa chafu hadi kwenye mapafu ili kutolewa nje ya mwili.

9. Maji huzisomba taka chafu toka sehemu mbalimbali za mwili hadi kwenye Ini na Figo ili kutolewa nje.

10. Maji ni mhimu ili kulainisha sehemu zote za mwili, hivyo kuzuia kufunga choo.

11. Maji huzuia shambulio la moyo na mshituko.

12. Maji ni mhimu katika kuupooza na kuupa mwili joto.

13. Nguvu za kiumeme katika maji hutupa nguvu za kufikiri, kufikiri kunahitaji nguvu, hivyo kuhitaji maji.

14. Maji ndicho kiamusho au kichangamusho (pick-me-up) pekee bora cha miili yetu kuliko kinywaji kingine chochote duniani, bila madhara.

15. Maji yatakurudishia usingizi wa kawaida na mororo, kila tuotapo ndoto mbaya au za kutisha (nightmares), mwili huwa unatuamusha kwenda kunywa maji. Jaribu hii, siku yeyote ukiota ndoto ya kutisha, amka na kunywa glasi moja ya maji kisha rudi kulala.

16. Maji huzuia uchovu, huwapa vijana nguvu. Fikiri: unapokuwa na uchovu na ukaamua kuoga, baada ya kuoga sehemu kubwa ya uchovu hupotea. Hapo umeoga tu, je ukiyanywa maji yenyewe?!!.

17. Maji hutengeneza ngozi nyororo hivyo kuzuia kuzeeka mapema.

18. Maji yatausawazisha katika hali yake ya kawaida mfumo wa uzarishaji damu kwenye mifupa, hivyo kuzuia Leukemia na Anaemia.

19. Maji yatapunguza maumivu ya ishara za kutokea kwa hedhi.

20. Upungufu wa maji mwilini huzuia uzarishwaji wa homoni za kiume na kike, hii ndiyo sababu ya kwanza ya uhanithi (impotence) na kukosa hamu ya tendo la ndoa (negative sex libido). Kuna tatizo kubwa linaendelea kwenye jamii yetu la upungufu wa nguvu za kijinsia hasa upande wa kina baba na kwa sehemu kubwa ni matokeo ya upungufu wa maji na chumvi mwilini.

21. Kunywa maji kutakutofautishia hisia za njaa na kiu ya maji, kunywa maji kwa muda na upunguze uzito na unene bila kuacha kula (dieting).

22. Maji yatazuia homa za asubuhi kwa mama mjamzito.

23. Maji yataunganisha mawazo na kazi za mwili, yataongeza uwezo katika kutambua malengo na nia.

24. Maji yatageuza utegemezi kwa vilevi ikiwa ni pamoja na pombe, kafeina na baadhi ya madawa ya kulevya.

25. Maji huzarisha nguvu za kiumeme na nguvu za kisumaku katika kila seli ya mwili – nguvu za kuishi. Nguvu za kiumeme zinafanya kazi kama nguvu za kisumaku na kuvipanga vitu anuwai kama sumaku hivyo kutoa uwepo wake sahihi na kujihusisha na matendo ya kikemikali.

26. Maji yanatumika katika kuvikatakata vyakula kuwa vipande vidogovidogo na hatimaye umetaboli au umeng’enywaji wake.

27. Maji yatakiongezea nguvu chakula (yaani maji ni transfoma chocheo ya chakula) na hatimaye chakula kutoa nguvu kwa mwili wakati wa umeng’enywaji wake.

28. Maji yataongeza uchukuwaji wa viini lishe mhimu vilivyomo kwenye chakula. Hii ina maana gani? Ni hivi, unapokula chakula na hauna maji ya kutosha mwilini basi ni viinilishe vichache tu ndivyo vitachukuliwa na mwili wakati sehemu nyingine kubwa ya chakula itabaki kama takataka tu.

29. Maji ni kilainishi kikuu kwenye maeneo ya maungio (joints) na hivyo kuzuia ugonjwa wa yabisi na kupooza.

30. Maji hutumika kwenye ‘diski’ za uti wa mgongo kuzifanya zigongane na kufyonza maji.

31. Maji huzuia kuzibika (clogging) kwa ateri kwenye moyo.

32. Maji huzuia kupunguwa kwa umakini na usikivu kwa watoto na watu wazima (Attention deficit disorder – ADD).

33. Maji huongeza ufanisi katika kazi.

34. Maji yatazuia mfadhaiko, pupa na kukata tamaa.

35. Maji huzuia ugonjwa wa Glakoma.

36. Maji yataiyeyusha damu na kuizuia isigande wakati wa mzunguko wake.

37. Upungufu wa maji unavihifadhi vijidudu nyemelezi (free radicals) mwilini, na maji ndiye muondoaji mkuu wa vijidudu hivi nyemelezi.

38. Maji hutoa nuru na mng’aro kwa macho na kuhimili kuona kwa sababu kushughulika na taarifa za mwanga kunahitaji nguvu nyingi katika kusafirisha taarifa toka mfumo mmoja katika jicho kwenda katika mfumo mwingine kwenye ubongo ili kutafusiriwa.

39. Maji na mapigo ya moyo vinatengeneza muyeyuko na mawimbi ili kuzuia vitu visivyotakiwa kubaki kwenye mkondo wa damu.

40. Mwili wa binadamu hauna hifadhi (store) ya maji, ndiyo maana unatakiwa kuyanywa kila siku.

41. Kunywa maji halisi, safi na salama kwa kanuni sahihi, kunausafisha mwili, maji yanaiacha sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (colon) kuwa na uwezo zaidi wa kutengeneza damu mpya (fresh blood) ijulikanayo katika lugha ya kitaalamu kama ‘Haematopaises’, kwamba difu la utumbo mkubwa na utumbo mdogo (mucousal fold) huamushwa upya kwa njia hii.

Ifike mahala tuache mazoea ya kuipa miili yetu maji ya mgawo (yaani tunapokunywa maji baada ya kusikia kiu).
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad