Imefichukaaa..Hii Ndio Sababu Kuu Amabyo Haisemwi Kuhusu Ujio a Waziri Mkuu wa Ethiopia...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn anatarajia kufanya ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini leo, Machi 31 na Aprili 1.

Ziara hiyo ni mwaliko wa Rais John Magufuli kwa Dessalegn kufuatia mazungumzo waliyoyafanya huko Addis Ababa, Ethiopia baada ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika (AU).

Akizungumzia ziara hiyo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba amesema baada ya kuwasili nchini, Waziri Mkuu huyo atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Magufuli na baadaye ujumbe wa Ethiopia na Tanzania watakaa pamoja na kuzungumza.

 Dk Kolimba amesema viongozi hao watashuhudia utiaji saini mikataba mitatu katika maeneo ya biashara, uwekezaji, utalii na diplomasia.

 "Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja na kujadili fursa za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara," amesema Dk Kolimba.

 Siku itakayofuata, Aprili Mosi, Dessalegn atafanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam na baadaye siku hiyo ataondoka kurejea Ethiopia.

 Dk Kolimba amesema Ethiopia imeonyesha nia ya kufungua ubalozi wake hapa nchini. Kwa sasa Ethiopia inawakilishwa nchini na Balozi wake aliyepo Nairobi, Kenya.

Dessalegn alitembelea Tanzania mwaka 2015 na kushiriki uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa za kuulia viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria. Pia, alishiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Magufuli zilizofanyika Novemba 2015.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad