Meya wa Ubungo Amfungulia Mashtaka Matano Makonda...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amemfungulia mashitaka matano Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo ameyawasilisha kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya Makonda ni pamoja na kughushi vyeti, kupokea zawadi bila kutangaza, jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma, kujipatia mali kutoka kwa watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya, kuwadhalilisha watu kwa kuwataja kwenye tuhuma za madawa ya kulevya bila kuwa na vielelezo na kutumia madaraka vibaya.

Hatua hiyo ya meya Jacob, imekuja siku chache baada ya mkuu huyo wa mkoa, kudaiwa kuvamia kwenye ofisi za Clouds Media, kushinikiza kipindi kilichorekodiwa kikiwa na habari ya Mchungaji Josephat Gwajima, kirushwe hewani wakati kipindi cha Shilawadu kikiendelea.

Kitendo hicho kilimlazimu Waziri Nape Nnauye, mwenye dhamana ya kuwalinda waandishi wa habari, aunde tume maalum kuchunguza sakata hilo, ambayo ilipewa muda wa saa 24 kukamilisha kazi yake, lakini mpaka sasa bado ripoti yake haijatoka.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Apelekee upuzii wake huko. Hamna lolote bali. Upupu tu. Utamwasha mwenyewe. Hivi hili Taifa Hawa wanaowania uongozi sijui kama wana mema miyoni mwao. Mtu akijitokeza akafanya mema atapigwa vita weeeee!!!!!!!! Mpka




    ReplyDelete

Top Post Ad