Mwakyembe Amkomalia Lissu Kugombea Urais wa TLS..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


WAZIRI wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa.

Alisema kama wanataka hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha wanasheria.

Dk Mwakyembe alikuwa akizungumza hayo na wageni wa TLS, waliomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma jana, wakiongozwa na Rais wa chama hicho anayemaliza muda wake, John Seka.

“Kama wizara hatujui mwelekeo wa TLS kwa sasa, hatuwezi kuiacha TLS ikijiingiza katika siasa halafu tukawaangalia tu. Hatuna nia ya kuitawala TLS, ila tunawajibika kuwasimamia kwa kuwa Sheria yenu iko chini yetu, mkiharibu kwa lolote wizara ndio yenye wajibu wa kuwatolea maelezo katika hilo mnalotaka kulifanya sasa kuna mgongano wa maslahi, je, ninyi kama wanasheria hamkuliona au hamlioni?” Alihoji Mwakyembe.

Wagombea wa TLS Mmoja wa wanasiasa wanaowania urais wa TLS ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye juzi alisema kitendo cha kukamatwa baada ya kufutiwa kesi, kina nia ya kufifisha harakati zake za kuwania urais wa TLS wiki ijayo, huku akitishia kugoma kula, endapo hatapelekwa mahakamani mapema.

Lissu ambaye ni mbunge kwa tiketi ya Chadema, alikuwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akituhumiwa kutumia lugha ya uchochezi katika kampeni za uchaguzi Jimbo la Dimani, Zanzibar.

Mbali na Lissu, wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo inayoshikiliwa na Rais wa sasa, John Seka ni kada wa Chadema, Lawrence Masha na aliyewahi kuwa rais wa chama hicho mwaka 2011 hadi 2013, Francis Stolla.

Wengine ni Godwin Mwapongo na Victoria Mandari. Uchaguzi wa chama hicho unatarajia kufanyika Machi 18, mwaka huu na mawakili 6,000 watapiga kura kumchagua Rais mpya wa TLS.

Ufafanuzi wa Mwakyembe Alisema Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila ni lazima wafahamu kwamba viongozi wanaowachagua ambao ndio watakaobeba sura ya TLS na mwelekeo mzima wa chama kama wanataaluma hawapaswi kuwa na nasaba za kisiasa ili kuepusha mgongano wa maslahi unapoweza kujitokeza.

“Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila tatizo linakuja pale mnapotaka kuchagua viongozi ambao tayari wanazo kofia mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vya siasa,” alisema na kuongeza: “Hao ndio watakaobeba sura na mtazamo au mwelekeo wenu hapo hatuwezi kukubali kwa kuwa watatenganishaje uongozi wao katika chama husika na uongozi wao ndani ya TLS, huo sasa ndio mgongano wa maslahi. “Ndio maana mwanasheria yeyote akiingia katika utumishi wa umma uwakili wa kujitegemea anauweka pembeni ili kuepuka mgongano wa maslahi.”

TLS sasa imekua na haihitaji muangalizi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma nchi ilipopata uhuru, kwani ina wasomi wengi na vijana wengi wamekuwa wanachama pia na kwa hiyo ni bora tuifute hii Sheria yenu na tuwape mwanya mkajisajili kama NGO ambako kiongozi yeyote wa chama cha siasa anaweza kuwa kiongozi wao,” alisema.

Aliwataka wafahamu kuwa dhamira ya Serikali ni njema huku ikizingatiwa kwamba sheria kama zilivyo taaluma nyingine nchini, bado zinahitaji uangalizi hasa ukizingatia uingiaji wa nchi katika utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Sifuni Mchome alisema kila taaluma ina namna ya uangalizi wake. Alisema kama wanasheria lazima kuhakikisha hatutoi vipaumbele kwa siasa, kama zilivyo fani nyingine nchini.

Alitaka wajiulize kama kweli hawauoni mgongano wa maslahi, huku wakizingatia kuwa wanapaswa kuhudumia jamii ya watanzania bila ya kuwabagua.

“Kama wanasheria lazima tuhakikishe hatutoi vipaumbele kwa siasa kama zilivyo fani nyingine, jiulizeni kama kweli hamlioni jambo hilo kama ni kikwazo huku mkizingatia kuwa tunatakiwa kuhudumia jamii bila ya kuwabagua sasa tukijiingiza katika siasa tutaihudumiaje jamii husika? TLS kutojihusisha na siasa ni miongoni mwa kanuni za kutuimarisha kama wanataaluma,” alisema Profesa Mchome.

Alisema Wizara ipo kuiangaliaTLS, na ndicho ilichofanya.

“Tupo hapa kuwaangalia, na ndicho tulichofanya, tumewashtua jamani mnaenda wapi? Hatuna nia mbaya ila tunawataka muwe katika mstari, hivi kweli kamati ya uchaguzi haijaona kama kuna mgongano wa maslahi hapo?

Alisema Serikali haitasita kuchukua hatua ya kuifuta Sheria ya TLS, kama chama hicho kitaendelea na msimamo wa kujihusisha na masuala ya siasa au kiuharakati.

Alisema chama hicho hakina budi kuangalia namna kinavyoweza kujikwamua katika hilo.

Kama hamuwezi kuendeleza misingi ya kitaaluma ya kutojihusisha na siasa au vyama vya siasa, basi serikali haitakuwa na namna zaidi ya kuifuta sheria ya TLS na TLS ya sasa itabidi ikajisajili kama NGO ili iendeleze harakati zake; na Serikali itaunda sheria nyingine itakayoanzisha chombo kitakachosimamia misingi ya kitaaluma.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad