Eheee...Simba Wamficha Niyonzima Dar,Yanga Wahaha Usiku na Mchana Kumtafuta...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


UKISEMA Simba wamemficha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, utakuwa hujakosea kabisa kwani tangu kumalizika kwa mpambano wa watani hao wa jadi hajaonekana tena uwanjani.

Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1, Niyonzima ni moja ya wachezaji ambao walishindwa kuonyesha kiwango kizuri na kuwafanya mashabiki kuondoka uwanjani vichwa chini.

Kiwango cha chini alichokionyesha Niyonzima katika mchezo huo kilisababisha mashabiki wa Yanga kuanza kukumbushia miaka iliyopita alipokuwa akihisishwa mapenzi yake ndani ya Simba.

Tangu mchezo huo dhidi ya Simba, Niyonzima hajaonekana tena na kikosi cha Yanga kwenye mechi na Ruvu Shooting pamoja na ile ya juzi ya Mtibwa Sugar, l

Uchunguzi uliofanywa  umebaini kuwa sababu kubwa ya kuondolewa Niyonzima katika kikosi cha Yanga ni mechi ya Simba.

Kwa sasa Mrwanda huyo aliyejiunga na Yanga Julai 2011 akitokea APR, ameonekana kukosa nafasi katika kikosi cha kocha Mzambia, George Lwandamina, huku kukiwa na taarifa kuwa wapo kwenye mpango wa kumsajili Kenny Ally kutoka Mbeya City ili awe mbadala wake.

Wakati mashabiki, viongozi na wanachama wa Yanga wakimwondoa kiungo wao mchezeshaji kikosini kwa madai ya kuwa na mapenzi na Simba, daktari wa kikosi cha Wanajangwani, Edward Bavu, amesema kuwa Niyonzima amekosekana katika mechi hizo mbili kutokana na matatizo  yakifamilia.

“Niyonzima hana tatizo la kiafya isipokuwa hakuweza kuwepo kwenye mechi hizi mbili zilizopita kutokana na matatizo ya kifamilia ambapo uongozi una taarifa hizo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad