AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi, ameondolewa katika wadhifa huo na kurejeshwa jeshini.
Akithibitisha habari hizi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu (DAS), Titus Mughuha, amesema Kanali Mkisi alitoa taarifa za uhamisho huo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na kusema kuwa, anarejea makao makuu ya jeshi alikokuwa awali kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
‘Ni kweli Kanali Martin Mkisi amepata barua ya kurudi makao makuu ya jeshi, uhamisho huo ni wa kawaida na haupaswi kuhusishwa na uzushi ama sababu zozote,” alisema Mughuha.
Kutokana na mabadiliko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani humo, Kanali Marko Gaguti, atakaimu nafasi hiyo hadi uteuzi mwingine utakapofanyika kujaza nafasi hiyo.
Kanali Martin Mkisi amedumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi tisa, akitokea makao makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutokana na uteuzi wa Rais, Dk. John Magufuli kwa wakuu wa wilaya 139 alioufanya Juni, mwaka jana.
Credit: Mtanzania
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
mmh yan hawa waandishi wetu ni sheeeeedah ndo maana trump aliwaita ni wachochezi
ReplyDelete