Rungwe Amkalia Kooni Makonda Sakata la Vyeti..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya utata wa jina lake unaozidi kuvuma mitandaoni

Utata huo unadaiwa kutokana na mkuu huyo wa mkoa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne kujiendeleza kielimu. 

Rungwe ametoa ushauri huo  kupitia kipindi cha maswali na majibu cha Kikaangoni , akimsisitiza Makonda kuweka ukweli mezani na kuacha kupiga chenga za mchangani kwa maana akiendelea kukaa kimya watu wanazidi kuamini uvumi huo.

"Namshauri Mkuu wa mkoa ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi" Amesema Rungwe

Pia, amemtaka kuacha kulia madhabahuni, kwakuwa hilo halitamsaidia kwa kuwa kulia siyo jibu, na atambue kuwa ofisi hiyo aliyopo sasa siyo yake bali ni wananchi, hivyo kila alichokikuta atakiacha.

"Siku moja nafungua 'ipad' yangu namuona Mkuu wa Mkoa analia mbele ya kanisa halafu mchungaji anambembeleza kama mjukuu wangu, mimi namwambia kulia kwake hakusaidii kitu yeye anapaswa kusema ukweli tu kama hilo jina siyo la lake halisi ila ni la kisanii sisi tutamuelewa". Alisema Rungwe

Kwa upande mwingine, Rungwe ambaye ni wakili msomi, ametoa ushauri wa kisheria kwa watu wenye ushahidi na suala hilo kwenda mahakamani kwa kuwa sheria inaruhusu mashtaka binafsi, ingawa bado Jamhuri itahitajika zaidi kuisimamia kesi hiyo.

Aidha Rungwe aliendelea kufunguka kwa kumtaka Makonda kuacha kung'ang'ania nafasi ambazo anastahili katika nafasi hiyo huku akimpiga kijembe kuwa mwanaume hachagui kazi aende akabebe hata zege kama hana ujuzi wa kufanya.

Kwa upande mwingine Mzee Spunda amemuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala hilo kama alivyofanya kwa maafisa wengine wa serikali.

Rungwe alilazimika kutoa ushauri huo kutokana na swali aliloulizwa kuhusiana na maoni yake kuhusu vita dhidi ya dawa kulevya ambapo amesema kuwa anaunga mkono vita hiyo, isipokuwa njia iliyotumika ya kutaja majina ya watu hadharani bila uhakika, haikuwa nzuri.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Unaitwa Hashim,pengine dini yako hamlii madhabahuni lakini Kwa mkristo kulia madhabahuni ruksa.

    ReplyDelete
  2. Mkristo kulia madhabahuni kwa namna hii kunaita ufarisayo na usadusisi. We mkrito usilete mambo ya uongo ya kugombanisha dini hapa. Mimi ni mkristo pia. Soma Biblia kwa utambuzi ukipewa vipaji vya Roho Mtakatifu. Wengi mnasoma hajui. Huyu ni kati ya Wale wanaosali mbele za umati watu wawaone ingawa wanamakosa. Wanajificha. Yesu anasema uwe mkweli. Linalofumbika duniani yeye analiona. Makonda si mkweli. Pia yesu anasema Tubuni. Yeye anajiosha tu mbele za watu. Thawabu zake ndo hizi amegundulika, hawezi ficha tena. Kajiumbua mwenyewe.Acheni mambo ya dini ya uchonganishi. Huku kumwita mtu mwislamu, badala ya kumwita jina ni uchonganishi wa kidini ambao hatuutaki nchini hasa kupitia Makonda mwenye vyeti feki.
    Hapa wote ni Watanzania, weka dini pembeni na ulaghai.

    ReplyDelete

Top Post Ad