Siku 14 Ngumu kwa Serikali ya Zanzibar...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Hatua ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutoa siku 14 kwa Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) na taasisi za Serikali kuhakikisha wanalipa madeni yao ya umeme la sivyo watakatiwa umeme, vitaipa wakati mgumu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka aliwaambia waandishi wa habari kwamba shirika lake linadai wateja hao jumla ya Sh275 bilioni.

“Tunadai kiasi kikubwa sana cha fedha kutoka kwa wateja wakubwa na wadogowadogo, mpaka Zeco, hivyo tunatoa notisi ya siku 14 kuanzia leo (jana) walipe deni lao kwani baada ya hapo tutasitisha huduma pamoja na kuchukua hatua nyingine za kisheria,” alisema Dk Mwinuka.

Katika kiasi hicho, Zeco inadaiwa Sh127 bilioni ambacho ni sawa na asilimia 15 ya Bajeti ya Serikali ya Zanzibar kwa mwaka 2016/17 ambayo ni Sh841.5 bilioni.

Pia kiasi hicho ni kikubwa karibu mara nne ya kile kilichotengwa katika bajeti hiyo kwa ajili ya mikopo ya ndani ambacho ni Sh33.0 bilioni hali inayoonyesha kwamba Zeco na SMZ watalazimika kuandaa mpango mkakati wa kulipa deni hilo ambao utamaanisha kujifunga mkanda ili kulimaliza.

Alipoulizwa kuhusu notisi hiyo ya kulipa deni, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Zanzibar, Salama Aboud Talib ambaye alikuwa ziarani Pemba alisema hadi jana hakuwa amepokea barua kutoka Tanesco hivyo asingeweza kuzungumza chochote.

Wiki iliyopita, akiweka jiwe la msingi katika kituo cha kupoza umeme cha njia ya Kv 132 mkoani Mtwara, Rais John Magufuli aliiagiza Tanesco kuwakatia umeme wadaiwa wote sugu ikiwamo Zanzibar. Alisema shirikia hilo halipo kisiasa, hivyo wadaiwa wote wakatiwe umeme.

Sambamba na hayo, alilitaka shirika hilo kutoingia mikataba na kampuni zinazoweza kusababisha au kuongeza madeni, badala yake mwekezaji yeyote akitaka kuwekeza azalishe umeme wake na kuuza mwenyewe.

Wadaiwa wengine

Kuhusu wadaiwa wengine, Dk Mwinuka alisema hadi kufikia Januari, shirika hilo lilikuwa linazidai wizara na taasisi za Serikali kiasi cha Sh52 bilioni huku kampuni binafsi na wateja wadogo wakidaiwa jumla ya Sh94 bilioni.

Alisema malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya shirika kwa wakati ikiwamo uendeshaji, matengenezo ya miundombinu pamoja na miradi mbalimbali.

Alisema kulipwa kwa malimbikizo hayo ya madeni kutaisaidia Tanesco kujiendesha kiushindani na kwa ufanisi zaidi, hivyo kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme nchini.

Alipoulizwa kuhusu mashirika na taasisi za umma zinazodaiwa malimbikizo hayo ambayo Tanesco haikuyataja, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas alisema mashirika hayo yanatakiwa kuanza kutekeleza agizo hilo kwa kulipa deni kama wanavyodaiwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad