Zijue Hatua Mbili Muhimu Katika Kusimama Kwa Uume Kabla ya Kufanya Mapenzi..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.
Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION


JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA.
1. HATUA   YA  KWANZA:

DAMU  KUTIRIRIKA  KWA  KASI KUINGIA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME  NA  KUUFANYA  UUME  KUSIMAMA  NA  KUWA  MGUMU.

Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu iliyopo  kwenye  ubongo,  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo, ambayo  nayo  hupeleka  taarifa  hadi  kwenye  mishipa  ya  uume. Taarifa  inapofika  kwenye  mishipa  ya  uume  huifanya  mishipa hiyo  ku-relax  na  hatimaye   kufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka  na  kutanuka. Mishipa  ya  ateri  inapo  tanuka  na  kufunguka, huruhusu  damu  kuingia  kwa  kasi  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  huume  kusimama.

Ni  muhimu  kujua  kuwa, mishipa  ya  uume  inapo relax  hupelekea  kuisukuma na  hatimaye  kuiziba  mishipa  ya  vena  iliyo  karibu  na  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuiondolea  uwezo  wa  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.

N.B: Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine  za  mwili.  Au  kwa  lugha  nyingine  unaweza  kusema, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.


2. HATUA  YA  PILI  :

DAMU  KUENDELEA  KUHIFADHIWA  KATIKA  UUME  WAKATI  UUME  UKIWA  UMESIMAMA  NA  HIVYO  KUUFANYA  UUME  UENDELEE  KUDUMU  KATIKA  TENDO LA NDOA   KWA  MUDA  MREFU.

Uume  ulio  simama, ili  uendelee  kusimama, ni  lazima  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo   wa  kunyonya  damu  kutoka  katika  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyinginezo  za  mwili. .
Mishipa  ya  Vena  ndio  inayo  husika  na  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume na  kupeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.  Ili  uume  uendelee  kusimama  lazima  mishipa  hii  ya  vena  iwe imezibwa. Ili  iweze  kuzibwa   ni  lazima  misuli  laini  ya  kwenye  uume  iwe - ime  relax na  hivyo  kuifanya  mishipa  ya  vena  kushindwa  ku  nyonya  damu  kutoka  kwenye  uume.

Endapo  mishipa  ya  vena  itazibuka , basi  itanyonya  na  kutoa  damu yote  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume uliosimama  na  kuipeleka  sehemu  nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  huo ulio simama  na  utasinyaa  mara  moja.


JINSI  UUME  UNAVYO  SIMAMA  NA  KUSISIMKA.

Tumeisha  zifahamu  hatua  mbili  muhimu  katika  kusimama  kwa  uume
Jinsi  Uume  unavyo  simama: Katika  uume  kuna chemba  yenye  mishipa  laini  sana, ambayo  ndio  huufanya  uume  kusimama.
Mishipa  hii  ipo kama  sponji  hivyo  huweza  kunyauka  na  kutanuka.
Damu  inapoingia  ndani  ya  mishipa  hii  huufanya  uume  kusimama  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.
Damu  inapoendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  mishipa  hii  wakati  wa  tendo  la  ndoa, huufanya  uume  uendelee  kusimama.
Mwanaume  unapo  patwa  na  wazo la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu  iliyo  kwenye  ubongo  hupeleka  ishara  kwenye  uti  wa mgongo, ambao  nao  hufikisha   taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume.
Taarifa  ikisha  fika  kwenye  mishipa  ya  uume, huifanya  mishipa  ya  uume  ku-relax  na  mishipa  ya  uume  inapo  relax, hufanya  mambo  makuu  mawili;
i.                   Kwanza  hufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka na  hivyo  damu  kutiririka  kwa  kasi  sana  kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume
( Mishipa  ya  ateri  ndio  inayo  tumika  kama  njia  ya  kuingiza  damu  kwenye  uume. Bila  mishipa  ya  ateri  imara  na  yenye  afya, damu  haiwezi kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, na  damu  isipoweza kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, basi  uume  hauwezi  kusimama )

ii.                 Pili huibana  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuizuia    kunyonya  damu  kutoka  kwenye  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu nyingine  za  mwili. Matokeo  yake  kuufanya  uume  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa. 
Kumbuka ,kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  neva  iliyo  karibu  na  mishipa ya  uume, ni kunyonya  damu kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu  nyingine  za  mwili. Kwa  lugha  nyingine, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume ulio simama.

Kadri  damu  inavyo  zidi  kuingia  ndani  ya mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo  zidi  kuwa  mgumu  na  kukakamaa.

Na  kadri  damu  inavyo  hifadhiwa  ndani  ya  mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo endelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa kwa  muda  mrefu.

Baada  ya  kumaliza  kufanya  tendo  la  ndoa,mishipa  ya  uume inarudi  katika  hali  yake  ya  kawaida (inanyauka ), ikisha  nyauka, mishipa  ya  ateri  inanyauka  pia, vena  zinafunguka  na  kunyonya  damu  katika  mishipa  ya  uume  na  kuirejesha  katika  sehemu nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  kurudi  katika  hali  ya  kawaida  ( Flaccid ).
Hali  hii  itaendelea  kujirudia  kwa  kadri  utakavyo  kuwa  ukiendelea  kufanya  tendo  la  ndoa.

Mambo  Muhimu  Katika  Kuufanya Uume  Usimame na  Kuendelea  kudumu  katika  kusimama  kwa  muda  mrefu wakati  wa  tendo  la  ndoa.
Ili  uume  uweze  kusimama  imara  kama  msumari na  uendelee  kusimama  imara  na  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo la  ndoa, ni  lazima  mambo  yafuatayo yawepo.

1.          Mishipa ya   uume iliyo  imara  na  yenye  afya  njema.
2.          Mfumo   mzuri  wa damu  katika   mwili  mzima.
3.          Mtiririko  imara  wa  damu kuingia  na  kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume.
4.          Ushirikiano  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume.

Ili  mwanaume  aweze  kuwa  imara  katika  tendo  la  ndoa, ni  lazima  mambo  manne  niliyo yataja  hapo  juu  yawe  sawa  sawa  bila  hitilafu  yoyote. Kinyume  chake, mwanaume  hawezi  kuwa  na  nguvu  za  kiume.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad