Baada ya Kuteuliwa Jana..Kitila Aweka Historia Hii Nchini..Chadema Watoa Tamko la Kumdhihaki..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MSHAURI wa Chama cha ACT Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo, ametangaza kuachana na siasa na kuwa mtumishi wa umma kwa asilimia 100.

Jana Rais John Magufuli, alitangaza kufanya mabadiliko madogo katika safu ya Makatibu wakuu na kumteua Profesa Mkumbo kushika nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Mbogo Mfutakamba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Profesa Mkumbo alishukuru kwa uteuzi huo na kueleza kuwa unapopewa kazi na Mkuu wa nchi kinachopaswa ni kuwajibika kwa niaba yake.

“Nimeipokea kuwa ukipewa kazi na Mkuu wa nchi unaheshimu kazi, unaheshimu aliyekua kazi yake, unaifanya kwa bidii kadri Mungu alivyokujalia, name nitafanya hivyo,” alisema na kuongeza:

“Mimi ni mtumishi wa umma, kiutumishi rais ana mamlaka ya kuwatumia kwa kadri anavyoona, nadhani ameona nitaweza kutumikia kwenye nafasi hiyo, namshukuru Rais, Namshukuru Mungu, basi nakwenda kuitumikia,” alisema.

Kuacha siasa kwa asilimia 100

Mkumbo alipoulizwa juu ya kuwa na ‘damu’ ya siasa, alisema kuanzia sasa anasimamisha shughuli za kisiasa na kuwa mtumishi wa umma kwa asilimia 100.

“Mambo ya kisiasa kwa sasa itabidi yasimame, nimsaidie Mheshimiwa rais kuhakikisha nchi hii inapata maji  kama anavyotarajia na sera za serikali zilivyo,” alifafanua.

Aprili 17, mwaka jana, Mkumbo alikaririwa na vyombo vya habari kuwa “Huu utaratibu wa kuwateua wasomi tu ambao ni walimu na wanataaluma kutoka vyuo vikuu hasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) si mzuri maana rais haoneshi kuwaandaa wengine kuchukua nafasi zao, tuachwe wasomi tufanye kazi za kitafiti na kitaaluma.”

Alipoulizwa juu ya kuikosoa serikali alisema “Hoja yangu kubwa ilikuwa ni kwamba serikali inapoteuwa ni lazima iajiri, lazima kuwe na ‘replacement’.”

Kitila ambaye amewahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, alipoulizwa tafsiri ya uteuzi huo kwa upinzani, alisema “ni heshima kwamba mtu mmoja ambaye alikuwa mpinzani anateuliwa maana yake kuna wapinzani wenye sifa za kiutumishi.”

“Pia ni kumshukuru rais kuwa ana uwezo wa kuvuka mipaka, amevunja ile miiko kwamba ni lazima utoke chama flani. Mtu kama mimi amenipa mtihani lazima nikaishi kama mtumishi wa umma kama ambavyo taratibu na sheria zinazopaswa kuwa,” alibainisha.

Atakalosimamia

Alisema maji ndilo hitaji namba moja la Watanzania na kwamba atafanya kazi kwa bidii kuhakikisha wananchi wanapata maji kama inavyotakiwa.

Katika kundi la Whatsapp la ACT Habari, wanachama walihoji uongozi wa ACT jinsi walivyopokea uteuzi huo na kama Profesa Kitila ameupokea.

Afisa habari wa ACT wazalendo, Abdallah Khamisi, aliulizwa wameupokeaje uteuzi wa Profesa, alijibu “vuteni subira”

Mnyika: Imedhihirisha alikuwa mamluki

Mjumbe wa kamati Kuu ya Chadema, John Mnyika, alisema uteuzi wa Profesa Kitila kuwa sehemu ya serikali unadhirisha ilikuwa sahihi kufukuzwa Chadema.

“Huo uteuzi umedhihirisha maamuzi yaliyofanywa na kamati Kuu ya Chadema ya kumfukuza uanachama kutokana na usaliti yalikuwa ni sahihi, kwamba alikuwa anatumika na utawala,” alibainisha Mnyika.

Mwaka 2013, Profesa Kitila, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto na Samson Mwigamba, walifukuzwa Chadema kwa madai ya kukiuka Katiba, sheria na kanuni za chama hicho.

Credit - Nipashe

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad