Baraka The Prince Awaonya Mashabiki wa Kiba Wasimpangie cha Kufanya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanamuziki wa RnB anayetamba na ngoma ya 'Acha Niende' Baraka The Prince amewaonya mashabiki wasimpangie maisha binafsi na kwamba wao kinachowahusu kutoka kwake ni muziki mzuri, video pamoja na kuwaandalia Show za kuwapa burudani.
Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio Barakah ametoa kauli hiyo baada ya siku kadhaa kushambuliwa na baadhi ya mashabiki ambao walimuita msaliti kwa kuonekana amepiga picha na meneja wa msanii anayetafsiriwa kuwa ni hasimu wa msanii mwenzake kutoka katika lebo yao ya Rock Star 4000. "Wewe kama ni shabiki wangu wa muziki haimaanishi pia ni shabiki wa maisha yangu binafsi, maisha yangu binafsi mniachie. Shabiki wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha? kama mtu niliyepiga naye picha ni binadamu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea". Amesema Barakah The Prince.
Katika hatua nyingine Baraka ameweka wazi kuwa tangu kusajiliwa katika lebo ya Rock Star chini ya Bi. Seven Mosha kumemuongezea nafasi na wigo mpana wa kujulikana ndani na nje ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani kubwa katika maisha yake.
Kwa upande mwingine Barakah amekanusha tetesi za yeye kutengwa katika lebo hiyo. "Unajua kwenye kampuni kila mtu ana makubaliano yake na mikataba yake, Lady Jaydee ana mkataba tofauti na mimi na pia kazi zinaenda kwa muda. Huu ulikuwa muda wake wa kuachia albamu lakini mimi nilikuwa na 'promote kazi yangu mpya hivyo watu wasiseme kama Rock Star inanitenga kwani hawajui mkataba wangu uko vipi. Wao wakae tuu na kusubiri kazi nyingi" Alisema Barakah The Prince.
.
TOA MAONI YAKO HAPA
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad