Dodoma: Wabunge wa CCM 'Vidomodomo' Kwisha Habari Yao..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jana, hapa Dodoma, kimefanyika kikao cha Wabunge wote wa CCM. Wabunge hao wanajumuisha Mawaziri, Manaibu Mawaziri,Spika, Naibu Spika na Wabunge wa kawaida watokanao na CCM. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri Mkuu. Kikao kilifanyika kwa mafanikio na mwitikio mkubwa.

Katika kikao hicho, ajenda zilikuwa kedekede lakini kubwa ni mbili. Kwanza, ni kuhusu bajeti na namna na kuipitisha. Baada ya mjadala mpana, ikaagizwa kuwa bajeti isikwamishwe na Wabunge wa CCM. Wabunge 'wameruhusiwa' kukosoa na kuiponda bajeti ya Wizara yoyote lakini waiunge mkono kwa asilimia 100.

Ajenda kubwa ya pili ilikuwa ni 'tabia isiyovumilika' ya Wabunge wa CCM kuikosoa 'waziwazi' Serikali na kuonesha kutuhumu vyombo vya dola. Hapa palikuwa na majadiliano yasiyo na mfano. Wabunge walisema kwa kuhema; walifoka na kutishia kutoka na wengine waliponda wasiowapenda. Lakini, likatolewa agizo lenye msisitizo kuwa Wabunge wa CCM wasivuke mipaka.

Viongozi waandamizi wa kichama na wa Wabunge wa CCM wameagizwa kufuatilia nyendo za Wabunge wote wa CCM na kuwachukulia hatua kali watakaovuka mipaka. Wabunge wa CCM wamekumbushwa kuwa wao ni wamoja na ni wao na chama chao ndio wanauunda Serikali iliyo madarakani. Wakosoaji wameonywa na kutakiwa kuwa makini.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama wewe ni CCM kweli, kuikosoa na kukishauri chama chako ni sawa lakini sio hadharani, kutafuta misifa........ hovyooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad