Hataree..Waziri wa Katiba Akiuka Amri ya Rais Magufuli Kuhusu Katiba Mpya..Afunguka Haya Kuhusu Katiba Mpya Ambayo JPM Alisema Sio Kipaumbele Chake..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale.

Prof. Kabudi amesema hayo wakati alipokutana na Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, amesema kuwa hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la Katiba Mpya, ingawa anajua mambo mengine kuhusu mchakato huo ambao wakati wa maandalizi yake alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. 

Amesema kuwa mchakato wa Katiba mpya uko pale pale hivyo pindi mchakato huo utakapo kamilika kwenye ofisi yake atauwasilisha kwenye kamati hiyo.

Aidha, Prof. Kabudi ameongeza kuwa ana muda mfupi katika wizara hiyo na kwamba, hajapata muda wa kukutana na mabosi wake akiwamo Waziri Mkuu, ili wazungumzie suala la Katiba Mpya.

Hata hivyo, amesema kuwa mchakato huo unahitaji umakini mkubwa hivyo atafanya kazi kulingana na utaratibu wa kisheria ili liwe na mwanzo na mwisho mzuri.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad