JE ni Lazima Kutokula Nyama Katika Siku ya Ijumaa Kuu?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

LEO ni Ijumaa Kuu. Siku ambayo Wakristo kote duniani wanaadhimisha kumbukumbu ya mateso na kifo cha Yesu Kristo msalabani.

Kanisa katika moja ya amri zake, linahimiza waamini hususan Wakatoliki kutokula nyama katika siku hii. Hata hivyo, wapo baadhi ya watu wanaoamini kuwa, ni lazima kuacha nyama katika siku hii huku wengine wakiamini tofauti. Pata jibu sahihi katika makala haya yaliyoandikwa na Joseph Sabinus.

Katika jamii nyingi, nyama ni miongoni mwa vyakula vya starehe. Ndivyo inavyoaminika kwa watu wengi. Hivyo, hapana budi kujua kuwa, maana ya msingi ya kutokula nyama katika Ijumaa Kuu, ni moja tu, kufunga starehe. Ijumaa Kuu ni siku ya mateso na kifo cha Yesu Kristo.

Katika mazungumzo na Katibu Mtendaji (Mkuu) wa Idara ya Liturjia wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Paul Chiwangu alisema kwa Mkristo Mkatoliki, kula nyama katika Ijumaa Kuu ni dhambi maana Kanisa linahimiza kujinyima siku hii ili kuyakumbuka mateso na kifo cha Yesu Kristo.

Katika moja ya machapisho ya gazeti la Kiongozi linalomilikiwa na TEC, Padri Titus Amigu aliwahi kuandika akisema, “Mateso hadi kifo cha Yesu msalabani, yamempata kutokana na dhambi zetu hivyo nasi tunakusudia kuacha starehe zetu na tunafunga ili tujutie dhambi zetu.”

“Hii ni kusema kuwa, tunafunga ili tutubu dhambi zetu na Mungu atuonee huruma na kutusamehe dhambi zetu na wengine ambao ni wadhambi kama sisi maana, kufunga, ni mapambano baina yetu na dhambi pamoja na mkuu wa dhambi yaani shetani.”

Injili ya Marko 6:26 inasema kwamba, katika kesi na masuala fulani, shetani hatoki pasipo sala na kufunga. Padri Amigu ambaye ni miongoni mwa wataalamu wabobezi wa Biblia anaandika kuwa, katika suala la kufunga, inampasa mtu kuchagua kitu kizuri cha kukiacha.

Anasema, “Kwa mfano, huwezi kufunga kitu kama kula ugali wa muhogo wakati ugali wa namna hiyo kwako ni shida, bali unafunga kitu kizuri kama labda kula wali na pilau. Huko ndiko kweli kufunga, kujikatalia na kujitesa kwa toba.”

Akaongeza: “Ieleweke kuwa, tangu enzi zile za kale, huko ilikoanzia dini yetu na huko kulikoanzia kufunga, waamini waliacha kula nyama na vitu vitokanavyo kama vile siagi na maziwa kwa vile vilikuwa ni vitu vinavyochukuliwa na kueleweka kuwa ni vya anasa na vile vilivyowakilisha anasa vilipopatikana.”

“Hilo, ndilo tulilolipokea kutoka kwa wamisionari kwamba, tunapofunga tuache kuvitumia vitu vya anasa na starehe; nyama ikiwa kitu kimojawapo.”

Kimsingi, kwa vile vitu vya starehe hapa duniani sio nyama pekee yake, kila mwamini anaalikwa kukagua vitu vyake vya starehe na hivyo, navyo tuviache siku ya kufunga apate muda zaidi wa kuhuzunika na dhambi zetu tukiomba toba kwa Yesu Kristo aliyesulubiwa kwa ajili ya dhambi zetu.

Kadhalika, katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya, Padre Amigu aliyekuwa Mkuu wa Seminari Kuu ya Peramiho Jimbo Kuu Katoliki la Songea, alisisitiza kuwa, mbali na sababu za kiimani katika dini, pia ipo sababu nyingine ya kibinafsi inayowafanya watu wengine wafunge kula nyama siku kama ya leo.

Akasema, “Hii ni ile sababu ya kufananisha nyama ya kuliwa na mwili au nyama ya Yesu Kristo aliyepigwa mijeledi na kutobolewa na kuchubuliwa na kuachwa akivuja damu nyingi. Hii ni hali inayowafanya wengine, washindwe kula nyama wakiona maiti ya mtu yeyote.”

Akasisitiza kuwa, hii ni sababu ya kibinafsi kwa kuwa Kanisa linapowasisitiza waamini kufunga kula nyama katika Ijumaa Kuu, lina hoja moja kubwa na ya msingi, ile ya kuacha starehe na kufunga na, siyo hiyo nyingine ya kuona nyama kama kitu kinachofanana na nyama au mwili wa Yesu Kristo ambayo kimsingi haina nguvu.

Kwa msingi huo katika Ijumaa Kuu pamoja na kuacha kula nyama tuache starehe zetu, mambo yanayotuvutia ili tukumbuke dhambi zetu na kutubu toba ya dhati inayotoka ndani ya moyo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pasaka inayozungumzwa katika Biblia ni Passover sio Easter, kanisa la Roman Catholic kwa makusudi walipotosha maandiko na kuingiza mambo mengi ya kipagani kanisani.
    Hakuna fundisho ktk Biblia linalitutaka tusile nyama siku ya pasaka, kama lipo naomba mniambie linatoka ktk kitabu gani.
    Mwisho napenda kuwakumbusha kuwa kila mtu anapaswa kusoma Biblia na kufanya maombi kwani dunia iko ukingoni na siku moja Mungu atatuhukumu kulingana na maisha tuliyoishi hapa duniani.
    Kwakuwa Mungu hakutuacha hivihivi, aliyupatia maandiko matakatifu kutuongoza (Biblia) hebu na tuisome na kuifuata tuachane na mafundisho yasiyo na msingi ktk Biblia.

    Biblia imeweka wazi namba ya kuadhimisha pasaka na Yesu kama kielelezo alitufundisha, sasa sijui imekuwaje watu wamebadili.

    ReplyDelete

Top Post Ad