Kajala Atinga Kortini Kudai Talaka..Mumewe Atoka Jela na Kumchunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja anadaiwa kudai talaka kwenye Mahakama ya Wilaya Kinondoni huku kisa kikuu kikitajwa ukimya wa mumewe, Faraji Chambo baada ya kutoka gerezani miezi ya karibuni, Amani limeambiwa.
Kwa mujibu wa chanzo, mara baada ya mume wake kutoka jela alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka saba kwa kosa la kutakatisha fedha kabla ya kushinda rufani, amekuwa hasomeki kwenye ndoa yake jambo ambalo linamfanya Kajala ashindwe kujua hatima yake.

SIKIA CHANZO
“Iko hivyo, sasa baada ya kuona mumewe hasomeki, hakuna vikao vya kuzungumzia ndoa yao na pia hajawahi hata kumuona tangu atoke jela, ndipo Kajala akapiga mahesabu kichwani na kuona njia ya amani kwake ni kushika talaka mkononi.


Kajala akiwa na mumewe, Faraji Chambo walipofunga ndoa yao.
“Unajua kwa nini anataka talaka? Kwa sababu Kajala kama mnavyomjua au kumwandika mara kwa mara, ni mwanamke anayependa sana kujirusha, sasa kuna wakati mwingine anakuwa na wanaume baa.
“Hii ina maana kwamba, kama hana talaka, siku moja mumewe akimtokea baa na kumbamba anaweza kusema amemfumania. Na ni kweli, ukizingatia kwamba, hajamwacha. Sasa unadhani ikitokea hivyo si itakuwa aibu kwa Kajala kwamba amefumaniwa!
“Ndiyo wapambe wa mjini wakamwambia wewe omba talaka, ukishakuwa na talaka yako mkononi utaishi kwa furaha zaidi.
“Siku zile mume wake akiwa jela, Kajala alikuwa anaweza kujiachia popote pale na wanaume kwa sababu hakuna wa kumfumania, sasa jamaa yupo nje, ” kilisema chanzo hicho.



YATAJWA KUWA SIRI NZITO
Hata hivyo, chanzo hicho kilisema kuwa, Kajala amekuwa akifanya siri kubwa kwenye ishu hiyo, kwamba hataki aonekane anadai talaka kwa ndoa iliyofungwa kanisani.

KAJALA ASAKWA KWA KUPEWA HAKI
Kama weledi wa taaluma ya habari inavyotaka, Amani lilimsaka Kajala ili kumpa haki ya kujibu tuhuma hizo ambapo alisema:
“Watu bwana, wanasema sana. Watu wanapenda kusema hata mambo binafsi ya watu ambayo hayapo. Mimi sidai talaka mahakamani, nitakaa hivihivi tu.”

Hivi karibuni, Kajala aliwahi kuripotiwa akisema kuwa, tangu mumewe atoke gerezani hajawahi kumuona na hajui hatima ya ndoa yake hivyo kuzidi kushibisha madai hayo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad