Kama ni Kweli Hili la Chuo cha DIT, Basi Watanzania wa Kudunduliza Wasahau Elimu ya Juu..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


nimepitia maeneo ya DIT kumwona mtoto wa rafiki yangu asomaye chuoni hapo akiwa mwaka wa kwanza. Mimemkuta kajiinamia kama anaongea peke yake. 

Nilivyomuuliza kulikoni kanijibu nina hati hati ya kurudia mwaka. Nikamuuliza umefeli? Akasema hapana,nmechelewa kumalizia ada ya chuo.

Nikamuuliza,umechelewa au hujalipa? Akaniambia hivi...wakati najoin mwaka jana,nililipa nusu kama ilivyokawaida ya wanachuo tunaokosa mikopo na nusu iliyobaki nmelipa juzi lakini wahasibu wamegoma kupokea bank slip kuwa hadi niende kwa registrar, nmeenda kwa registrar kasema hawezi tena kuruhusu isipokuwa nirudie mwaka! Nikabaki nashangaa. 

Hivi mtu amelipa tayari pesa iko ndani ya akaunti ya chuo,anaambiwa arudie mwaka kisa kachelewa kulipa kwa wiki mbili!!! Sio kuwa mwaka umeisha na wala si kama ni wakati wa mitihani kazuiwa hadi alipe bali kachelewa kulipa na sio kwamba hajalipa! 

Sasa binafsi nmebaki nimeduwaa, hivi watanzania kwa pesa yetu ya kudunduliza mzazi kajichanga, kanyimwa mkopo amejibana akakamilisha bado tena mtoto anapata frustrations za kurudishwa aanze tena upya!!??

Nimejiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu! Hii ni kumkomoa au kumsaidia? Hii itakuwa ndo kumsaidia mtoto wa mtanzania apate elimu ya juu au wanaotakiwa wasome ni wale watakaopata mikopo na watoto wa matajiri tu?

Kabisa nimekosa majibu na nimeishia kumshauri akamuone mkuu wa chuo labda hajaelewa kilichosemwa maana itakuwa hatari.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii inadhalilisha maana ya Elimu ya bure. Kama unasadia watoto wa waTanzania wasio na uwezo wasome, halafu hawa aliofanikiwa wana shindwa kuendelea, umesaidia nini? Kwanini hawana 4 installments payment system ambazo vyuo na shule zingine wanazo. Unalipa kidogo kidogo badala ya nusu mbili inakuwa roborobo. Huku nchi za watu ndio wanyonge tunavyosomesha watoto otherwise tungeshindwa. Hii kweli ni nchi ya kutetea Wanyonge?
    Asante kwa Mwandishi kurusha habari hii, maana maudauku na conspiracy theories zinafunika taarifa za muhimu kama hizi. Vyama vya kutetea haki za wanyonge viko wapi?

    ReplyDelete

Top Post Ad