KIMENUKAA- Msanii wa Filamu Nchini Yusuph Mlela Amemtusi Rapa Nay wa Mitego

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KIMENUKAA---Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela amemtusi rapa Nay wa Mitego kwa kile anachodai kuwa msanii huyo anapotosha jamii juu ya maandamano waliofanya baadhi ya wasanii  wa filamu nchini.

Yusuph Mlela ambaye kwenye post yake ameonekana kushindwa kutumia lugha ya staha huku akionesha kutokwa na povu jingi kutokana na mapokeo ya mashabiki wa filamu ambao walio wengi wamekuwa wakiwachana wasanii hao na kuwataka kufanya kazi zenye ubora.

Rapa Nay wa Mitego alisikika akisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu ambao waliandamana ni matahira kwani kitendo cha wao kutaka filamu za nje zizuiliwe hakina tija na mantiki yoyote.

Kutokana na jambo hilo, ndipo hapo msanii huyo alipoamua kushusha ujumbe kwa msanii Nay wa Mitego

"Nay True Boy wewe jamaa si ulikuwa chocolaa wewe leo umeyapatia kidogo unasahau kwamba nyuma yako kuna kundi la vijana wanatamani kuwa waigizaji\wanamuziki wakubwa....acha kupotosha jamii yetu Kwa sababu zako binafsi... sisi wasanii hatujakataza movie za nje. Tunataka wanaozisambaza wafuate taratibu za kisheria ili uwiano wa biashara uwepo ndiyo lengo la maandamano"alisema Mlela


Mbali na hapo msanii huyo pia ameomba mpambano na Nay wazichape


"Nay wa Mitego acha kutafuta sifa... nakushangaa kuwa na ufikilivu mdogo kama wewe siyo msanii...halafu huwezi kufananisha filamu na muziki..... Wewe si mtoto wa Manzese unajifanya unajua kupiga ngumi nataka Round 3 tu za boxing kwenye stage ili Tanzania ijue nani taahira nikutie adabu..... This is serous coz we mtoto mdogo tu kwangu ** kuongea sana tabia za kike wewe si hip hop na unajiamini njoo uwanjani chagua popote pale" Yusuph Mlela .


TOA MAONI YAKO HAPA
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad