Mbunge Ataka Zanzibar Ipewe Fedha na Tanzania Bara ili Ilipe Deni la Umeme.,,!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Jaku Hashimu Ayoub ametaka makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali za Serikali yapelekwe Zanzibar ili kulipia deni la umeme. 

Jaku alisema hayo wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, ambapo alisema kuna kodi zinazolipwa Tanzania Bara, lakini hazipelekwi Zanzibar kwa ajili ya kusaidia maendeleo ikiwamo kulipia deni hilo.

 Mbunge aliyedai kuwa na ushahidi juu ya kauli yake hiyo na kwamba yupo tayari kuutoa, alisema fedha hizo ni muhimu zikapelekwa ili zisaidie ulipaji wa malimbikizo ya deni la umeme. 

Machi 9, mwaka huu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lilitangaza kuikatia umeme Zanzibar kutokana na limbikizo la deni la zaidi ya Sh275.38 bilioni. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema wameipa siku 14 kuhakikisha kuwa inalipa deni hilo. Hata hivyo, siku chache baadaye Tanesco ilitangaza kulipwa Sh10 bilioni kama malipo ya awali ili isikate umeme visiwani humo.

 Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Magomeni (CCM), Jamal Kassim Ali alitaka kujua iwapo Serikali haioni haja ya kodi ya mishahara (paye) kwa wafanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) isikusanywe visiwani humo kwa ajili ya kusukuma maendeleo. 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashantu Kijaji alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mapato sura ya 66, kifungu cha 4(a) na (b), kodi za kampuni ni za Muungano na zinakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 

Pia, alisema hata kampuni ambazo zimesajiliwa Tanzania Bara lakini zinafanya kazi Zanzibar, kodi zake zinakusanywa Bara. 

Naibu waziri alisema iwapo kampuni itakuwa imesajiliwa Zanzibar na ikawa na matawi Tanzania Bara inatakiwa kulipa kodi yake Zanzibar.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad