SABABU Usalama wa Taifa Kuchomolewa...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


UPANDE wa Jamuhuri umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuondoa kesi ya kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa na kujipatia chakula katika hoteli ya kimataifa jijini Arusha.

Kesi hiyo ilikuwa ikimkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mpinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha, Lengai ole Sabaya.

Akitoa ombi hilo mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Gwantwa Mwakuga jana, wakili wa serikali Grace Madikenya alisema upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo kwa sababu shahidi mmoja muhimu yupo nje ya nchi kwa miezi 18.

“Sasa tumeona tutamtesa mteja wetu, hivyo kwa nia njema kabisa tumeamua kuiondoa mahakamani kesi hii, maana miezi hii ni mwaka mmoja na miezi sita,”alisema.

Ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa utetezi, Edna Haraka ambaye aliiomba mahakama hiyo iendelee na kesi hiyo kwani upande wa mashitaka unatumia mhimili huo kama kichaka cha kumnyima haki mteja wake na kumnyanyasa.

Alisema upande huo hauna nia njema na mshitakiwa kwani itakuwa mara ya pili unaondoa shitaka hilo mahakamani hapo baada ya kufuta kesi, kumkamata tena mteja wao na kumnyima dhamana.

“Sasa leo tupo katika kusikiliza shahidi wa tatu na badala ya kuleta shahidi walileta maelezo ya shahidi," alisema Haraka. "Na leo wanakuja na stori ya kuiondoa ili waendelee kumnyanyasa mteja wetu.
"Hapana.

"Ofisi hiyo ya Mwanasheria Mkuu inatumika vibaya kwa kivuli cha mahakama.”

Edna alisema serikali ya sasa inasisitiza mpango wa kuharakisha mashauri kusikilizwa, wa BRN.

Hakimu Mwakuga alisema atatoa uamuzi wa kukubali ama kukataa ombi la kuiondoa mahakamani hapo Ijumaa ijayo.

Lengai anatuhumiwa kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa na kujipatia huduma ya chakula na malazi kwenye hoteli ya kimataifa ya Highway ya jijini Arusha.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad