Wafanyakazi wa Manji Wakimbia Jela...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


WAFANYAKAZI 16 wa kampuni ya Quality Group Ltd, wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. 500,000 au kwenda jela miaka mitatu baada ya kukiri makosa ya kufanya kazi nchini bila kibali. Jumla ya faini yote ni Sh. milioni 22.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, baada ya washtakiwa kukiri mashtaka yanayowakabili. Quality Group Ltd ni kampuni ya mfanyabiashara Yusuph Manji.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, alisema mshtakiwa wa kwanza hadi 14 wanakabiliwa na mashtaka matatu hivyo katika kila kosa kila mmoja atatoa faini ya Sh. milioni 1.5.

Pia alisema kama watashindwa kulipa faini hiyo, kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela katika kila kosa, hivyo watatumikia kifungo cha miaka tisa jela.

Kwa upande wa washtakiwa namba 15 na 16, Meneja mradi Jose Kiran na katibu wake, Prakash Bhatt, wanaokabiliwa na tuhuma za kukiuka amri ya ofisa uhamiaji na kujaribu kutoroka, wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. 500,000 au kwenda jela miaka mitatu. Wamekwepa kifungo kwa kulipa faini.

Jose na Prakash wanadaiwa kuwa Februari 20, 2017, wakiwa raia wa India na waajiriwa wa Quality Group Ltd, walimzuia ofisa wa Uhamiaji kufanya kazi zake na kwamba walikataa kuripoti katika ofisi za Uhamiaji zilizoko jijini Dar es Salaam kwa kujaribu kutoroka Tanzania kupitia mpaka wa Horohoro, Tanga.

Washtakiwa 14 waliobaki ni mshauri Jagadish Mamidu (29), mshauri Niladri Maiti (41), mshauri Divakar Rajasekaran (37), Mhasibu Mohammad Taher Shaikh(44), mshauri Bijenda Kumar (43) na mshauri Prasoon Kumar Mallik(46).

Wengine ni mshauri Nipun Dinbadhu Bhatt (32), Meneja Msaidizi Pintu Kumar (28), mshauri Anuj Agarwal (46), mshauri Varun Boloor (34), mshauri Arun Kumar
Kateel (46), mshauri Avinash Chandratiwari (33) na mshauri Vikram Sankhala (50). Nao walilipa faini na kukwepa vifungo hivyo.

Mahakama imesema ili waweze kuendelea kuishi nchini ni lazima wafuate sheria.

Wakili wa washtakiwa hao, Hudson Ndusyepo kabla ya hukumu kutolewa aliiambia mahakama mshtakiwa namba moja hadi 14 hawakuwa na nia mbaya ya kutenda makosa hayo.

Alidai kuwa walikutana na Afisa wa Uhamiaji wakamwambia wanahitaji kuongeza muda wa viza za kufanya kazi na wakamkabidhi hati zao za kusafiria na baadae aliwarejeshea zikiwa na visa ndani.

Aliendelea kudai kuwa wao waliamini viza hizo zilipatikana kwa halali na malipo yalifanyika na fedha kuingia Serikalini kupitia mpaka wa Tunduma, na kwamba risiti walipata.

Aliendelea kudai kuwa baada ya kukamatwa iligundulika viza hizo zilipatikana kinyume cha sheria.

Alieleza hilo ni kosa lao la kwanza na akaomba mahakama iwasamehe, wapewe adhabu ndogo na nafasi nyingine ya kuwepo nchini na kwamba watafuata taratibu za nchi hii.

Kwa upande wa Mwendesha Mashtaka wa Idara ya Uhamiaji, Method Kagoma yeye alidai kuwa washtakiwa hao waliingia nchini mwishoni mwa mwaka jana na wakapewa viza za miezi mitatu za kufanya kazi.

Alidai kuwa baada ya vibali hivyo kwisha walifanya wanavyojua, ikiwamo kutoa maelezo ya uongo na kufanikiwa kujipatia viza hizo.

Kwa pamoja walidaiwa kuwa Februari 13 katika Kampuni ya Quality Group Ltd iliyopo wilaya ya Ilala, wakiwa raia wa India walikamatwa wakiwa na viza za kibiashara zilizoghushiwa.

Wanadaiwa kuwa Februari 13 katika kampuni hiyo ya Quality Group Ltd washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikamatwa wakiishi nchini kinyume cha sheria.

Iliendelea kudaiwa kuwa Februari 13 washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikamatwa wakifanya kazi katika kampuni ya Quality Group Ltd kama washauri bila ya kuwa na kibali kinachowaruhusu kufanya hivyo.

Washtakiwa waliachiwa baada ya kulipa faini zao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Swali ndiyo wameishalipa faini kwa kosa la kufanyazi nchini bila vibali vya kufanya TZ(working permit)sasa kinachofutia ni nini?Yaani ndiyo imetoka hiyo au watarudishwa kwao udosini

    ReplyDelete

Top Post Ad