Yafahamu Madhara 10 ya Kutisha Yanayotokana na Ulaji Mkubwa wa Chumvi Kwenye Chakula

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


tafiti zilizofanywa na jarida la new england journal of medicine nchini uingereza limegundua kwamba zaidi ya watu milioni moja na laki sita wanauawa na na ulaji wa chumvi kila mwaka, kifo ni hatua ya mwisho ya madhara ya chumvi lakini kuna madhara mengi sana yasababishwao na chumvi kabla ya kifo.

kitaalamu chumvi ni kompaundi au mchanganyiko wa element za sodium chloride, kemikali hii hutumika kuhifadhi chakula na kuleta ladha ya chakula, kemikali hii huweka kiwango cha maji mwilini sawa na kusaidia utumaji wa taarifa kwenye mishipa ya fahamu, husaidia kuhifadhi maji mwilini, ni muhimu kwenye damu ya mwili,kutengeneza tindikali kwa ajili ya mmengenyo wa chakula tumboni, hata dripi za maji tunazopewa mahospitalini hua zina chumvi.

maisha ya kisasa na vyakula viulivyopo vinawafanya watu kula chumvi nyingi sana kuliko zamani, hii husababisha madhara makubwa ambayo hayatibiki kirahisi.

kiafya mtu anatakiwa ale chakula chenye chumvi inayosikika kwa mbali sana na asiongeze chumvi chakula kinapokua mezani, hii ni sawa na gramu 1.5 mpaka 2.3 kwa siku, hii ni sawa na kijiko kimoja cha chakula kwa siku nzima.

ulaji mkubwa wa chumvi kwa wakati mmoja husababisha kuishiwa maji kwa seli, hii huleta kuchanganyikiwa, degedege, kupoteza fahamu na kifo lakini pia uwepo wa chumvi kidogo sana kwenye damu husababisha kuvimba kwa seli, kuchanganyikiwa,kupoteza fahamu na kufa..hii hutokana na unywaji mkubwa wa maji kupitiliza kiasi kwa wakati mmoja.

kimsingi vyakula vingi tunavyokula vina chumvi ya kutosha ambayo inatosha kabisa kuendesha mwili wetu bila kuongeza chumvi nyingine ya ziada, vyakula hivyo ni kama vitunguu,malimao,maji ya kunywa,viazi,ngano,nyanya,maboga,caroti, spinachi, kabechi,mapera, zabibu,epo,karanga,mayai, maziwa na vingine vingi

yafuatayo ni madhara ya ulaji wa chumvi nyingi ambayo yanaweza kua ya muda mrefu au ya muda mfupi.

yafuatayo ni madhara ya muda mrefu wa kula chumvi nyingi kwenye chakula...

presha ya damu; chumvi ina tabia ya kuzuia maji kutoka nje ya mwili kupitia mkojo, lakini pia kuna ushahidi kwamba kupunguza ulaji wa chumvi kwa wagonjwa wa presha hupunguza presha kwa wagonjwa wa presha.

kansa ya tumbo; utafiti umeonyesha kwamba nchi ambazo kuna ulaji mkibwa sana wa chumvi kama japani kuna wagonjwa wengi sana wa kansa ya tumbo la chakula ukilinganisha na nchi ambazo hazina ulaji mkubwa wa chumvi kama uingereza.

ugonjwa wa moyo; chumvi husababisha kuvimba kwa moyo na kuufanya kua mkubwa kitaalamu kama left ventricular hypertrophy, hii husababisha moyo kushindwa kusukuma damu kama unavyotakiwa kufanya kazi.

magonjwa ya figo; kupanda kwa presha ya damu husukuma damu nyingi sana kwenye mishipa ya damu, hii huharibu figo na kuifanya kushindwa kutoa maji mwilini lakini pia viungo muhimu kama macho na mishipa ya damu huharibika.

addiction; ulaji mkubwa wa chumvi humfanya mlaji kuendelea kupenda vyakula vyenye chumvi nyingi sana na kushindwa kabisa kuvumilia kula vyakula vyenye chumvi kidogo...hii hizidi kuathiri mwili na kuusababishia matatizo makubwa zaidi.

kiharusi; huu ni ugonjwa wa kupooza unaosababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu ya kwenye ubongo kutokana na mafuta au kuvujia kwa damu, kwa ulaji wa chumvi nyingi huongeza presha ya damu na kupasua mishipa midogo ya kichwa na kuleta kiharusi.

kuongezeka uzito; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba chumvi huzuia maji kutoka nje ya mwili, hii huongeza uzito wa mwili na kumfanya mtu kujisikia amejaa tumbo muda mwingi, kumbuka lita moja ya maji sawasawa na kilo moja ya uzito.

kupungua kwa uwezo wa mishipa ya fahamu; katika watu wenye umri mkubwa chumvi inazidi kupunguza uwezo wao wa kufanya shughuli mbalimbali na kujikuta wakitetemeka na kushindwa kubeba hata kikombe kimoja cha chai.

magonjwa ya mifupa; mwili wa binadamu unapoteza kiwango cha calcium mwilini pale mtu anapozidi kutumia chumvi zaidi, hii huweza kusababisha mifupa kua milaini na kuvunjika kirahisi pale inapoangukua kidogo tu.

mwili kushindwa kutoa mabaki mwilini; chumvi nyingi mwilini huingilia mfumo wa mwili kuondoa mabaki ya uchafu mwilini, moja ya mabaki yanayobaki ndani ya mwili ni uric acid ambayo inaweza kusababishwa ugonjwa wa maumivu makali ya jointi kitaalamu kama gauti.

suluhisho ni nini? punguza sana kiasi cha chumvi kwenye mla wako na baada ya muda utazoea, kwa wagonjwa wa presha ambao wanatakiwa wale chumvi kidogo zaidi kuna chumvi maalumu kwa watu hao ambazo zinapatikana mijini, chumvi hizi zina kiwango kidogo sana cha sodium hivyo presha zao huweza kushuka
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad