BAADA ya Kuzuiwa Kuchchua Mchanga wa Madini Nnje ya Nchi..Acacia Waanza Mchakato wa Kufunga Mgodi..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Uongozi wa kampuni ya Acacia, inayomiliki mgodi wa Buzwagi, jana ulitoa taarifa ya kupunguza wafanyakazi zaidi ya 100 wakati ikijiandaa  kufunga mgodi huo ifikapo mwaka 2020.

Meneja mahusiano wa kampuni hiyo, Nector Foya alisema kuwa taarifa ya kupunguza wafanyakazi ilitolewa baada ya meneja mkuu wa Buzwagi, Stewart Hamilton kuzungumza na wafanyakazi wa mgodi huo jana.

“Ni kweli taarifa hiyo imekuja baada mkurugenzi kuzungumza na wafanyakazi wa mgodi leo (jana),” alisema Foya.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa wafanyakazi 100 watapunguzwa baada ya kufanyika vikao mbalimbali katika wiki mbili, kuanzia jana ikiwa ni pamoja na kujibu maswali mbalimbali.

Mbali na upunguzwaji huo, taarifa inaeleza kuwa wafanyakazi hao watatoka katika idara zinazotoa msaada na huduma.

“Tutaanza mawasiliano na jamii zetu na kulenga matumizi yetu katika mradi endelevu ya jamii inayoweza kuchangia katika kuifanya jamii iweze kujitegemea baada ya 2020,” inaeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa inaeleza kuwa uchimbaji wa mgodi huo utaanza kumalizikia katika robo ya nne ya mwaka na uchimbaji utaishia mwisho wa Desemba 2017 na uchenjuaji utaisha 2020.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad