Fahamu Maana ya Ndoto Zinazohusu Nyoka..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


NDOTO NA NYOKA

Maana yake:-

Ndoto za Nyoka zinaashiria mtoto wa kiume, mtu asiyekuwa na heshima, Adui, mali iliyofichwa, ushirikina, mabadiliko, uwezo, kiongozi mbaya, na mwanamke.

Nyoka katika ndoto anawakilisha mtu anayeishi Bondeni, vilevile

Nyoka katika ndoto ni ishara ya uadui kutoka kwa wakwe zako au watoto au ni ishara ya uovu na wivu kutoka kwa majirani zako.

Ukiota unamuona nyoka maana yake ni kwamba utadanganywa na mkeo au mumeo.

Ukiota unapigana na nyoka ni ishara ya kuwashinda au kuwapindua adui zako.

Ukiota unakimbizwa na nyoka ni ishara ya uadui unaokujia kutoka kwa adui yako.

Ukiota umemuona nyoka mwenye vichwa saba ni ishara ya wewe kutenda dhambi au makosa makubwa.

Ukiota unamuona chatu anakushambulia ni ishara ya kwamba mwanamme au mwanamke mwenye uwezo ambaye ni adui yako atakusumbua sana. Kama ukiota ameshindwa kukuumiza maana yake utapewa sifa za uongo. Ukiota umemuuwa ni ishara ya kuwashinda maadui zako.

Ukiota nyoka amejikunja ni ishara ya kupatwa na hatari au kifungo. Pia ni ishara ya kupata maradhi na kuchukiwa na watu.
Ukiota nyoka amelala maana yake ni adui aliyelala hasa kwa mtu ambaye ni muovu.

Ukiota nyoka wa kwenye maji maana yake ni kwamba utapokea msaada au utapata uamuzi kuhusu jambo lako.
Ukiota unafuga nyoka au unamiliki nyoka hiyo ni ishara ya kupata uwezo au madaraka.

Ukiota nyama ya nyoka maana yake ni fedha za adui au ni ishara ya wewe kupata furaha.

Ukiota umevaa ngozi ya nyoka maana yake ni kwamba utamgundua adui yako.

Ukiota umemuua nyoka na damu yake ikakurukia kwenye mikono yako maana yake ni kwamba utamshinda vibaya adui yako.
Ukiota umemwona nyoka anauliwa barabarani hiyo ni ishara ya kutokea vita au magomvi.

Ukiota nyoka mdogo ni ishara ya matatizo kwa mtoto wako au mtoto yeyote unayemhudumia au kumsaidia.

Ukiota unawinda nyoka maana yake ni kwamba utamdanganya adui yako.

Nyoka mweusi katika ndoto ni ishara ya adui yako mwenye nguvu.

Nyoka mweupe katika ndoto ni ishara ya adui mnyonge.

Ukiota nyoka anakusemesha na anakuambia maneno mazuri maana yake ni kwamba utapata bahati ya kukaa vizuri na adui zako na utanufaika nao.

Ukiota nyoka anakusemesha na anakukaripia kwa maneno makali hiyo ni ishara ya kwamba adui yako atakutesa na kukunyanyasa.
Ukiota umegeuka nyoka ni ishara ya kwamba utatoka dini yako na kwenda dini nyingine.

Ukiota umegeuka nusu nyoka na nusu mtu huyo ni ishara ya kwamba utafanikiwa kupunguza nusu ya nguvu za adui yako.

Ukiota umegundua ngozi ya nyoka ambaye imetengenezwa kwa dhahabu maana yake ni kwamba utagundua mali iliyofichwa.

Ukiota nyoka anakumeza hiyo ni ishara ya kupata madaraka makubwa ya uongozi.

Ukiota nyoka amekukalia kichwnai hiyo ni ishara ya kupata heshima kubwa kutoka kwa watu wenye madaraka au viongozi.

Ukiota uwanja mkubwa uliojaa nyoka hiyo ni ishara ya kwamba itanyesha mvua kubwa ambayo italeta madhara.

Ukiota nyoka mwenye pembe ni ishara ya kupata mafanikio ya kibiashara.
Nyoka mweusi na chatu katika ndoto wanaashiria viongozi wa kijeshi.

Nyoka wa majini ni ishara ya pesa au utapata pesa.
Ukiota shamba lako limejaa nyoka ni ishara ya kwamba utapata mazao mengi msimu huo.

Ukiota nyoka anaondoka nyumbani kwako maana yake ni kwamba nyumba yako itavunjwa.

Ukiota umemuua nyoka ni ishara ya ndoa na vile vile utawashinda adui zako na wote wanaokuchukia.

Ukiota unakula na nyoka meza moja maana yake ni kwamba utatengana na rafiki yako.

Ukiota umemwona nyoka wa Jangwani maana yake ni kwamba mtavamiwa na majambazi.

TAFSIRI YA NDOTO 10 ZA KUMUONA NYOKA USINGIZINI

1.unapomuota nyoka amekufa,ni ishara Umeepushwa na uadui na shari yake

2-unapomuota nyoka mdogo ni biashara ya kupata mtoto

3-unapoota umemuuwa nyoka juu ya kitanda chako,utafiliwa na mkeo

4-ukiota umemuuwa nyoka kwa fimbo ni ishara ya kuwa utaowa

5-ukiota umemuuwa nyoka kwa jiwe ni dalili ya kupona sihri uliyonayo na kutoka kwa jini mwilini mwako

6-ukiota umemuuwa nyoka kwa upanga na kumgawa vipande v3 utamtaliki mkeo talaka 3

7-ukiota joka kubwa linajizongazonga mwilini mwako ni dalili ya jini aloingia mwilini anatafuta sehem ya kujificha ndani ako

8-ukiota nyoka anaungua kwa moto ni dalili ya kufanya kazi kwa kile kisomo cha Ruqya alicho fanyiwa mgonjwa

9-ukiota unafukuzwa na nyoka ni dalili ya kuwa jini aliekuingia hajakaa vizuri mwilini mwako,au ni jini afriti jini mbaya anakuandama

10-ukiota una nyoka shingoni mwako ukamkata kata utatoa talaka kwa mkeo

11. Kuota nyoka mara kwa mara ni dalili ya wewe una Jini mahaba ana kuandama mwilini mwako ukiwa ni Mwanamme utakuwa una jini Mwanamke anaye kuharibia nguvu zako za kiume na kukuharibia kazi na maisha yako yanakuwa ni magumu kila unacho kifanya hakiwi. Ukiwa ni Mwanamke unaota kila mara nyoka ni dalili ya wewe kuwa una jini Mwanamme Jini Mahaba anaye kutia mikosi na kukuharibia Wanaume na kizazi chako na maisha yako fanya umtoe haraka.

Credit - Mzizi Mkavu
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad