Gwajima Atema Cheche Sakata la Mchanga wa Madini...Ampa Makavu Live Tundu Lissu Juu ya Kuitisha Nchi ...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma. 

Mchungaji Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu na mali nyingi 

"Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima 

Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo 

"Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe madini hakuna kwenda" alisema Gwajima 
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hili jambo ni zito kulingana upeo wa kila mmoja wetu, mm ninachotaka kusema ni kwamba soko la madini haliko uingereza na pia siyo kwamba hawa wawekezaji ndiyo wanaweza kushawishi masoko ya madini yashushe bei dunia huo siyo uchumi ninaoujua mm maana yake ni nini kuna inchi Kama China inauwezo mkubwa tu kiuchumi kwa kuchirikiana na jumuiya zake Kama urrusi, afrika kusini Japan na nchi zingine za asia

    ReplyDelete

Top Post Ad