Kwa Mara ya Kwanza Nchi Imekuwa na ma-IGP Wawili..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu tumekuwa na maIGP wawili. Mmoja amepewa madaraka ya kuwa mkuu wa jeshi la polisi na mwingine amevuliwa madaraka hayo lakini amebaki na cheo chake.

Wengi hawajui kuwa IGP ni cheo na sawa na vyeo vingine kama Inspekta wa polisi au Mrakibu wa polisi au Koplo. Tofauti ni kwamba vyeo vya chini vinaweza kushikwa na watu wengi lakini cheo cha juu kabisa ambacho ni IGP hushikwa na mtu mmoja tu. Yani makoplo wanaweza kuwa wengi, makamishna wengi, mainspekta wengi lakini IGP mmoja.

Huyo IGP mmoja ndo hupewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi. Kumbuka kuna tofauti kati ya CHEO na MADARAKA. Mtu mwenye cheo cha IGP ndio hupewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi. Sasa kwa mara ya kwanza tumekua na watu wawili wenye cheo kimoja cha IGP.

Tofauti ni kwamba mmoja ameondolewa madaraka ya kuongoza jeshi la polisi, na mwingine kapewa madaraka hayo. Huyu aliyeondolewa madaraka, ameambiwa atapangiwa kazi nyingine. Lakini bado amebaki na cheo chake cha IGP. This means Mangu akiteuliwa balozi atatambulika kama Balozi IGP Ernest Mangu maana cheo chake hajavuliwa. Ni sawa na wale wanajeshi wanaoteuliwa kuwa wakuu wa mikoa, wanabaki na vyeo vyao.

Na kwa kuwa Mangu hajastaafu utumishi, siku akistaafu basi atastaafishwa kwa cheo chake cha IGP. Japo wakati huo anaweza kuwa na madaraka mengine kama ukuu wa mkoa, ubalozi etc.

SWALI: Je ni sahihi kuwa na maIGP wawili kwenye nchi? Yani watu wenye vyeo vinavyolingana japo wana madaraka tofauti. Hii iko sawa au mkuu amechemsha? Maana haijawahi kutokea tangu uhuru. Hebu wale ndugu zetu ambao ni askari watusaidie uelewa kdg.!

Malisa G
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad