Mrema - Gerezani Sio Hotelini Jamani...!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Mh. Augustino Lyatonga Mrema amewaonya wananchi kuacha kutenda makosa yatakayo wafanya kukataliwa kurudi kwenye jamii pindi watakapohitaji kupata msamaha 'Parole' na kusisitiza gerezani siyo hoteli.

Mapema wiki akifanya mahojiano EATV, Mhe. Mrema ameweka wazi kuwa hakuna mfungwa anayeweza kupatiwa msamaha na bodi ya Parole ikiwa tayari jamii yake haimtaki na kuongeza kuwa mfungwa atalazimika kutumikia kifungo chake.

Aidha Mrema ameongeza kwamba watu wamekuwa wakifanya makosa makubwa kwenye jamii hali ambayo inawanyima nafasi za misamahaa ambayo ni haki yao na kwamba tatizo linakuja wakati wakupata ruhusa kwa jamii anayoishi kukataa kutoa ruhusa.

"Huwa tunaauenda eneo analoishi au alipozaliwa kuwaeleza watu juu ya msamaha wanaotaka kuutoa na kama wakikataa kwa sababu na wao haki yao kukubali aua kukataa basi mtuhumiwa utarudishwa tu magereza. Nataka kuwaasa acheni kufanya mambo yatakayowafanya mkatliwe, jiepusheni na makosa yatakaowafanya mkose haki yenu labda itokee bahati mbaya" Mh. Mrema alifunguka.

Pamoja na hayo ameongeza kwamba jamii haipaswi kuwakataa watu wao walipo magereza kwani baada ya kumaliza kifungo watarudi kwenye maeneo yao na hawatakuwa na uwezo wa kuzuia waendelee kukaa magereza.

"Jamii inatakuwa ifahamu hawa watu waliopo magereza ni bdugu zao na ni watu wao. Tengezenezeni mahusiano mazuri na siyo kwamba mtu akishafungwa ndio anageuka mnyama mnatakiwa mtambue ni binadamu na ana haki zake zote za kimsingi" aliongeza Mrema.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad