Rasmi..Azam Fc Watangaza Kuachana na John Bocco..!!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC ya Tanzania John Bocco ameachana rasmi na klabu yake hiyo aliyoitumikia kwa muda mrefu kwa mafanikio makubwa.

Nahodha huyo wa zamani wa Azam FC na taifa Stars ameondoka Azam FC akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na matajili hao wa jiji la Dar es Salaam wakitumia dimba la Azam Complex.

Kwa mujibu wa uongozi wa Azam FC kupitia kwa afisa habari wa timu hiyo Jafar Idd Maganga wamethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo kwani hawakuwa na mkataba naye tena.

Amesema "Kimsingi Azam FC inatangaza rasmi kuwa kuanzia hii leo Bocco siyo mchezaji tena wa Azam FC", Lakini watamkumbuka kwa mengi mazuri aliyoifanyia timu hiyo mpaka ilipofikia.

Maganga maarufu kama mbunifu amesema Bocco yuko huru kujiunga na timu yoyote hii ni baada ya kumalizika kwa mkataba na hata mazungumzo baina yao kutofanikiwa hivyo wao wanamtakia kila la kheri huko aendako.

Tayari kumekuwa na taarifa za mchezaji huyo mrefu kusajiliwa na Simba taarifa ambazo bado yeye na hata viongozi wa Simba hawajawa tayari kuzungumzia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad