Mtabiri: Majini ya Madini Yanawamaliza Mawaziri wa Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, mtabiri maarufu nchini, Hassan Yahya Hussein, amesema sababu za mawaziri kutodumu katika wizara hiyo kunatokana na nguvu za majini zilizopo.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko ofi sini kwake, Magomeni Mwembechai Dar, mtabiri huyo alisema kinyota, madini asili yake ni majini, hivyo waziri yeyote anayepewa kitengo hicho lazima awe na nguvu ya maombi kwa Mwenyezi Mungu na awe amejitengeneza vilivyo.


Waziri wa Nishati na Madini ambaye Rais Dkt.John Magufuli alitenguliwa uteuzi wake, Profesa Sospeter Muhongo.
“Madini asili yake ni majini, hivyo anayesimamia hapo lazima awe na nguvu, kama hajajizatiti lazima uondoke tu, hata kama kosa siyo lako, unajikuta ukitumbuliwa kutokana na ushawishi wa majini,” alisema mtabiri huyo, mtoto wa gwiji wa utabiri Afrika Mashariki na Kati, hayati Yahya Hussein.

Akisisitiza kuhusu suala hilo, alisema inawezekana Waziri Muhongo hakuwa na makosa, lakini makosa yakawa ni ya watu wengine kutokana na kushawishiwa na majini, ndipo balaa likamwangukia yeye.

“Katika wizara ambazo ni ngumu kuziongoza kutokana na kuwa na nguvu za majini na mashetani ni Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Mali Asili na Utalii na Wizara ya Ardhi. Wanaoteuliwa kuongoza wizara hizo wanatakiwa kuwa makini sana kwa kumuomba Mungu au kujitengeneza kwa njia yoyote ili wawe na nguvu,” alisema.

Waziri Muhongo alitumbuliwa siku ambayo Rais Magufuli alipokea taarifa ya kamati ya kuchunguza mchanga wa dhahabu wa makontena 277 yaliyokuwa yamezuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa amri ya mkuu huyo wa nchi.


Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa Awamu ya Nne, William Ngereja.
Katika ripoti hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Mruma, ilibainika kuwa kulikuwa na madini mengi ya dhahabu, shaba na sulphur, katika michanga hiyo, tofauti na maelezo yaliyotolewa awali na Wakala wa Ukaguzi wa Madini, TMAA ambayo ni taasisi iliyo chini ya wizara, kitu kilichomfanya Rais Magufuli kuhoji usimamizi wa waziri katika kitengo hicho.

Baadhi ya mawaziri waliowahi kukalia wizara hiyo ni pamoja na Nazir Karamagi, Dk. Ibrahim Msabaha, William Ngeleja na Prof. Muhongo mwenyewe, ambao wote waliondolewa kwa kashfa tofauti na George Simbachawene aliyehudumu kwa muda mfupi baada ya Muhongo kuondolewa mwishoni mwa uongozi wa serikali ya awamu ya pili kwa kashfa ya Escrow.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad