MWALIMU Asimulia Safari Iliyoua Wanafunzi 32..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Lucky Vicent Academy waliyokuwa wanasoma wanafunzi 32 waliofariki dunia kwa ajali jana, Longino Vicent amesema ndiye aliyesimamia safari iliyosababisha vifo vya watoto hao na wafanyakazi watatu.

Vicent amesema wanafunzi hao na walimu wawili pamoja na dereva waliofariki, walianza safari yao saa 12:30 asubuhi kuelekea Karatu ambako watoto hao walipaswa kufanya mtihani wa kujipima uwezo na wale wa Shule ya Tumaini.

“Mimi ndiye niliyesimamia safari hiyo na niliwasafirisha waliondoka hapa saa 12; 30 asubuhi, sikufikiri kama yatatokea haya. Kila kitu kilikuwa salama tu,” alisema akisimulia walivyoanza safari watoto hao kabla ya gari walilopanda aina ya Toyota Costa lenye namba za usajili T 871 BYS kupinduka korongoni na kusababisha vifo hivyo.

Mwalimu Longino alisema shule hizo mbili zimekuwa na tabia ya kufanya mitihani ya ujirani mwema na kuwa hiyo ni mara ya tatu.

“Huu ni mwaka wa tatu, hata shule ya Tumaini huwa inakuja Arusha,” alisema.

Mwalimu huyo alisema shule hiyo ilikuwa ya kwanza kimkoa mwaka 2004 na ya 20 kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.

Wanafunzi hao waliofariki dunia walikuwa wakisoma shule hiyo ya bweni ambayo kwa mujibu wa wakazi wa Arusha ni miongoni mwa shule bora na iliyotoa mwanafunzi bora katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga alisema eneo la ajali lina kona nyingi na mteremko mkali na kwamba, kuna maeneo ambayo yamekuwa yakisababisha ajali kutokana na miundombinu yake ilivyokaa.

Aliyataja eneo jingine kuwa lipo barabara ya Morogoro kwenda Dodoma linaloitwa Makunganya lina utelezi mwingi na kuwasihi madereva kuwa makini sana wakati wa mvua. Wanafunzi waliofariki ni wa darasa la saba.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro alisema miili ya wanafunzi hao itaagwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid leo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama serikali insjua hili, kwa nini mdiweke umuhimu kuweka rami hapo kwanza? Viongozi wetu wa nchi hamna priorities.maafa mengi yanatokea sababu ya negligence. Kushindwa kufikiri na kuchukulia umuhimu wa maisha ya mtanzania. Mnanunua ndege za anda kwa mabilioni huku mkiwaaacha watanzania wengi wakisafiri duni. Raisi alikuwa ni waziri huko, leo anatoa mabilioni kwa usafiri wa watu wachache skiwaacha Watanzania bila usslama nadhifu wa baravara. Maombi hayatarufisha maisha ya watoto inafikia wakati serikali ipelekwe mahakamani kwa kutokuwajsli watanzsnia, na kuwafidia wazazi kwa neglegency kwa kuyaneglect matstizo kwa makusudi. Ijifunze. Sala na maombi hayasaidii, bsli majukumu kikazi yaboreshwe. Na yanapopuuzwa, serikali ichukuliwe sheria. Ndipo mtakomesha hili jambo.?

    ReplyDelete

Top Post Ad