MWANANGU ni Biashara, Msinipangie Cha Kufanya- Skyner Ally

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Skyner Ally  amewatolea povu watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Instagram wanaomnenea mabaya mtoto wake kuwa atakuwa jike dume kutokana na mavazi anayomvalisha yatawarudia wao na kwamba yeye anaendelea kutengeneza pesa.

Skyner ameamua kutoa povu hilo baada ya watu kum-'diss' namna anavyomvalisha mtoto wake wa kike huku wengine wakidai mtoto ataharibikiwa na kuwa jike dume kutokana na mavazi kitu ambacho kimemfanya Skyner kuweka wazi na kudai mtoto wake anamtumia kibiashara katika kuuza nguo zake na si vinginevyo.
"Wazazi na walimu wa instagram ifike pahala mniachie mwanangu, msiniingilie wala  kunipangia na hayo mnayomuombea mwanangu sijui atakuja kuwa jike dume Inshallah itawarudia nyie na vizazi vyenu  ifike pahala mnielewe nipo Instagram kibiashara sipo kwa ya ajili ya show off hapana"- aliandika Skyner.
Aidha Skyner ameongeza kuwa hawezi kutumia watoto wa watu wengine  katika kutangaza biashara yake wakati ana mtoto wa kufanya kazi hiyo pasipo kumlipia huku akidai mtoto wake ni wa kike japo kafanana na baba yake.

Huu ndiyo ujumbe aliouandika Skyner

"Huyu ni model wangu, Model wa biashara yangu. Nimchukue mtoto wa nani sasa anitangazie biashara yangu najua kuzaaa nimezaa na kulea pia nalea, lakini sura kachukua kwingne so sad. Nahitaji support yenu sana kwenye biashara yangu jamani namkubali tu kwamba huyu ndo Model wa biashara yangu atavaaa code zote ziwe za kike au za kiume kwa ajili ya biashara zetu mie na mwanangu niachieni mwanangu" - Skyner aliongeza



Skyner ambaye ni mama mzazi wa mtoto 'Munie' aliyezaa na mwanamuziki Nay wa Mitego amekuwa akimtumia binti yake katika kutangaza biashara zake zanguo katika mitandao ya kijamii kitu ambacho kimewafanya watumiaji wa mtandao huo kumjia juu kwamba anamuharibu mtoto kisaikolojia kutokana na aina ya mavazi anayomvalisha.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad