NOMA Sana..Mrembo Achomwa Visu na Mpangaji Wake, Kisa Kandambili za Chooni..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Aisha Salum, mrembo mkazi wa Kiwalani nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii alichomwa visu usoni na mpangaji mwenzake aliyefahamika kwa jina la Mama Mwantumu baada ya kutokea mzozo uliosababishwa na kandambili za chooni na kumfanya majeruhi huyo kushonwa nyuzi 36 wakati akipatiwa matibabu.

SAKATA ENEO LA TUKIO LILIVYOKUWA

Kwa mujibu wa mashuhuda eneo la tukio, nyumba wanayoishi watu hao, mara kwa mara imekuwa ikiingia katika manenomaneno juu ya kupotea kwa kandambili hizo, zinazowekwa na wapangaji hao kwa ajili ya kuingilia chooni. Kutokana na kupotea huko ambako wapangaji wamekuwa wakisema kuwa ni kwa kushangaza, baadhi yao walikuwa wakimtuhumu mpangaji mwenzao kutokana na tabia yake ya kutopenda ukaribu na wenzake.

Siku ya tukio inadaiwa kuwa majeruhi huyo alitoka nje ya chumba chake kwa lengo la kuelekea msalani, lakini alipotazama kandambili zake hazikuwepo eneo aliloweka mlangoni hapo, hali iliyosababisha awaulize wapangaji wenzake. “Nilipofika sikuyakuta malapa yangu, nikauliza yalipo lakini hakuna aliyenipa jibu. Badala yake kila mmoja akaanza kutoa malalamiko ya namna malapa yanavyopotea kimaajabu sehemu hiyo,” alisema Aisha.

MGENI ASABABISHA TIMBWILI

Bila kutambua, wenyeji hao wakiwa hawana hili wala lile, ndani msalani, alikuwepo mgeni ambaye ndiye aliyekuwa amevaa kandambili hizo na alipotoka, aliziacha mlangoni na kuelekea kwa mwenyeji wake, Mama Mwantumu. “Sasa sijui huko ndani mgeni alimwambia nini, maana alitoka nje akaanza kusema nani anamsema mgeni wake, tukamwambia hakuna aliyemsema, sisi tulikuwa tukiulizia malapa, akaongea sana, kukatokea kutoelewana kwa maneno,” alisema Aisha.

MAMA MWANTUMU ATAKA WAZICHAPE

Katika hali ya kushangaza, mama huyo alimtaka Aisha wachapane ili kumpata mshindi, lakini mrembo huyo alisema asingeweza kupigana na mwanamke huyo ambaye kiumri ni sawa na mama yake mzazi. “Mimi nilishangaa sana na kumwambia kuwa wewe ni mtu mzima sana ambaye unaweza hata kunizaa, siwezi kupigana na wewe, kitendo cha kumwambia hivyo tu, akanikumbatia kutaka kupigana, ndiyo watu wakaja kutushika, wakanitoa mimi nikaingia ndani kwangu,” alisema Aisha.

MAMA MWANTUMU AMVIZIA, AMCHOMA VISU

Inadaiwa kuwa baada ya Aisha kuingia ndani kwake kwa ajili ya kuepusha vurugu zaidi, mama Mwantumu naye aliingia ndani kwake kabla ya ndugu wa mrembo huyo kuwasili chumbani hapo na kumtaka kuondoka ndani ya nyumba hiyo kwa muda kuepusha mhemko. “Ile natoka tu ndani ya chumba changu, maana kimeangaliana na cha Mama Mwantumu, alitoka na kisu kisha akanichoma nacho usoni na kifuani, hivi ninavyoongea, nimeshonwa nyuzi 36 na bado sijatolewa kwa sababu nilikwenda hospitali iliyopo Buguruni inayoitwa Plan, ndiyo walinitibia toka mwanzo wa tukio, niliambiwa kidonda bado ni kibichi,” alisema Aisha.

SAKATA LATINGA POLISI

Baada ya kutibiwa, Aisha alikwenda kuripoti tukio zima Polisi Buguruni ambako lilifunguliwa jalada la kesi lenye namba KY/RB/427/2017 na mtuhumiwa alikamatwa na kushikiliwa kwa siku chache kabla ya kuachiwa kwa dhamana. “Mtuhumiwa alikamatwa na polisi akawekwa ndani kwa siku chache lakini alitoka kwa dhamana, ila tuliambiwa kesi itakwenda mahakamani siku mbili hizi,” (maneno haya aliongea Alhamisi), lakini hadi tunakwenda mitamboni bado mtuhumiwa alikuwa hajafikishwa mahakamani.

MTUHUMIWA AOMBA MSAMAHA

Katika kuonyesha kujutia kosa lake na pengine shetani aliyempanda kichwani, Mama Mwantumu alijikuta akilia baada ya kumuona majeruhi huyo akiwa na majeraha hayo na kuomba msamaha kwa kilichotokea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad