Steve Nyerere Afyata Mkia...Ajisogeza Kwa Mama Wema Sepetu Baada ya Kutofautiana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Muigizaji mkongwe wa Filamu Tanzania Steve Nyerere kati ya mambo aliyozungumza ni kuhusu kuyaweka pembeni mambo yote yaliyotokea baina yake na Mama yake Wema Sepetu.

Steve Nyerere amesema katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ameamua kusamehe na kusahau kila kilichotokea baina yao na lazima waanze upya kwa sababu hata Vitabu vya Dini vinaeleza.

"Lazima tusamehe ili kuanza mwanzo. Kwa hiyo, mimi nasema kwanza vile vitu vilipita – yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Yule ni Mama – ni Mama yangu, ni rafiki yangu, ni ndugu yangu, ni mwanafamilia. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
 “Mzazi haombi samahani; mzazi hakosei. Mzazi anapatia lakini mwenyewe ndani ya nafsi yake anasema pale nilimkwaza mwanangu au pale nilimkosea mwanangu. Naamini ndani ya nafsi yake anasema hapa nilimkwaza mwanangu au hapa nilimkosea mwanangu.” – Steve Nyerere.
.
.
TOA MAONI YAKO HAPA
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad