TRUMP Amtumbua Jipu Bosi wa FBI..Ni Baada ya FBI Kuchunguza Mahusiano ya Trump na Rais Putin wa Urusi..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais Donald Trump amemfuta kazi Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi (FBI), James Comey kutokana na namna alivyoshughulikia barua pepe za aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic, Hillary Clinton.

Hata hivyo, wanachama wa Democratic wamesema kuwa Comey alifukuzwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa inachunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubainika kwamba Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa Bunge la Congress wiki iliopita.

Rais Trump alimwandikia barua Comey kumwambia kuwa alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.

Sessions alisema kuwa Wizara ya Sheria ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu wa sheria na mwanzo mpya unahitajika.

Ikulu ya Whitehouse imesema mrithi wake atapatikana haraka.

Pamoja na hayo yote, kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Chuck Schumer amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad