Freema Mbowe Afunguka: Polisi Msituzibe Midomo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelitaka jeshi la polisi nchini kutowafunga midomo na kusema kitendo cha jeshi hilo kuwafukuza waandishi wa habari wakati wakifanya kazi yao si sawa.

Freeman Mbowe amesema hayo leo Alhamisi  baada ya jeshi la polisi kuwafukuza waandishi wa habari ambao walikuwa wakifuatilia tukio la kuwasili kwa Mhe. Edward Lowassa Makao Makuu ya Polisi ambapo leo alikwenda kuitika wito wa jeshi hilo baada ya juzi kutoa maelezo na kutakiwa kufika leo tena.

Mhe Edward Lowassa alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi siku ya Jumanne tarehe 27 kufuatia kauli zake alizozitoa ambazo zinasemakana kuwa ni uchohezi

Lowassa juzi alifika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kutoa maelezo yake kwa muda wa masaa manne, kisha baada ya hapo alijidhamini mwenyewe na kutakiwa kufika siku ya Alhamisi ya tarehe 29 Julai 2017 ambapo amefika na kuambiwa uchunguzi wa jambo lake haujakamilika hivyo arudi tena tarehe 13 Julai 2017.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad