Mali za Rafiki wa Ivan Bongo Zakamatwa, Aingizwa Kwenye Sakata la Madawa ya Kulevya..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Majanga! Lile sakata la tuhuma za kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’ lililowagusa watu wa kada mbalimbali, wakiwemo baadhi ya mastaa wa Bongo kwa majina yao kutajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa, miezi kadhaa iliyopita, limemkumba rafiki wa aliyekuwa mume wa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, marehemu Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Patrick Christopher ‘PCK’ (29).
BREAKING NEWS

‘Breaking news’ zilizolifikia Risasi Jumamosi zilieleza kuwa, kufuatia tuhuma hizo, mali za msanii huyo ambazo ni nyingi kiasi cha kushangaza kutokana na umri wake mdogo, zinadaiwa kukamatwa jijini Dar. Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kilidai kuwa, katika orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar, jina lake liliingizwa kwenye listi ya kwanza iliyotolewa na mkuu huyo, lakini hakuwepo nchini hivyo aliporejea ndipo akajaa kwenye mikono ya polisi na sasa kesi yake hiyo, tayari ipo mahakamani

“Mali za PCK zinashikiliwa yakiwemo magari matatu, Toyota Prado (shilingi milioni 60), Nissan Murano (shilingi milioni 45) na Toyota V-Mark (shilingi milioni 32) na nyumba ya ghorofa ya kifahari iliyopo maeneo ya Kigamboni (Dar) jirani kabisa na Ufukwe wa Bahari ya Hindi huku akaunti zake zote za benki zikifungwa kutokana na kuwa kiasi kikubwa cha fedha hadi kesi yake itakapomalizika kwa sababu inasemekana mali hizo siyo za halali.

“Unaambiwa sasa hivi jamaa ana hali ngumu mno maana kesi iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (Dar) huku hati ya kusafiria na vitambulisho vyake vyote vikiwa vimeshikiliwa na haruhusiwi kutoka nje ya Jiji la Dar.

“Kiukweli jamaa anatia huruma maana unajua mtu ukishazoea maisha ya kitajiri na uhuru ni vigumu sana kuwa sawa pale unapokosa hivyo vitu. “Mali zake zimekamatwa kwa kuwa inasemekana siyo za halali kwani haijulikani anafanya biashara gani ambazo zinaweza kumwingizia kipato kikubwa kiasi hicho hivyo anachunguzwa ndiyo maana zinashikiliwa,” kilisema chanzo hicho.

RISASI JUMAMOSI LAMSAKA

Baada ya kunyaka ishu hiyo, Risasi Jumamosi lilimsaka PCK kwa siku tatu hadi alipopatikana ambapo alibanwa hadi akakubali kufunguka. Msanii huyo anayetamba na Nyimbo za Nitazame Usoni na Sweet Baby aliyomshikisha Mwanamuziki Barnaba Elias alikiri mali zake kushikiliwa na akaunti zake kufungwa huku akieleza kuwa, hawezi kuzungumza zaidi kwani atakuwa anaingilia uhuru wa mahakama.

“Ni kweli mali zangu zimeshikiliwa yakiwemo magari na nyumba iliyopo Kigamboni. Pia vitambulisho na hati za kusafiria zimeshiliwa. Siwezi kusema ni shilingi ngapi zilizopo benki wala siwezi kuzungumzia sana ishu hii maana tayari iko mahakamani Kisutu,” alisema PCK.

NI RAFIKI WA IVAN

Risasi Jumamosi lilimweleza kuwa, lilitonywa kwamba ni rafiki wa marehemu Ivan hivyo kumtaka kufafanua juu ya hilo ambapo alifunguka: “Ni kweli Ivan alikuwa ni rafiki yangu sana. Ndiye aliyenitoa kwenye maisha ya ziro mpaka hivi nilivyo sasa na ukaribu wetu ulikuwa mkubwa sana. “Niliishi naye jijini Kampala Mtaa wa Munyonyo (Uganda) kati ya mwaka 2000 na 2001.

“Mwaka 2002, Ivan alihamia Afrika Kusini, nikabaki Kampala, ilipofika mwaka 2004, aliniita huko (Afrika Kusini) nikawa nimehamia. Mwaka 2007 niliamua kurudi Bongo kwa sababu ndiyo nyumbani na kuanza kujitegemea mwenyewe, lakini bado urafiki na biashara zetu ziliendelea na muda mwingi tulikuwa wote Afrika Kusini kwenye biashara zetu wiki kadhaa zilizopita kabla ya kuumwa na kufariki dunia.

“Nimeanza kuhaso na maisha haya muda mrefu sana. Huwa sichagui kazi ya kufanya hivyo nafanya biashara mbalimbali kwa kusafiri nje ya nchi kama Uingereza, China, Afrika Kusini na kwingineko. Pia nafanya Muziki wa Bongo Fleva.”

MSIKIE MWANASHERIA WAKE

Risasi Jumamosi lilizungumza na mwanasheria wake anayesimamia kesi hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Musa Ngonyani ambaye alisema mteja wake huyo anashitakiwa kwa kumiliki mali haramu. “Kesi inaendelea Mahakama ya Kisutu na namba yake ni CC 247/2017 na inaendeshwa na Hakimu Kihawa na itatajwa tena Juni 13, mwaka huu.”

MAMLAKA YA MADAWA YA KULEVYA

Akizungumzia kinachoendelea juu ya vita dhidi ya madawa ya kulevya, Afisa Habari wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Florence Bahati Khambi alisema kuwa, vita hiyo inaendelea na hakuna ambaye atabaki salama, awe muuzaji, mtumiaji au yeyote yule.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad