‘Mjane wa JPM’ Aangukia Pua Tena Kortini..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kwa mara nyingine mama aliyeangua kilio mbele ya Rais John Pombe Magufuli (JPM) akidai kudhulumiwa mirathi ya marehemu mumewe, ameangushwa tena mahakamani, baada ya Mahakama ya Wilaya ya Tanga kutupilia mbali kesi dhidi ya wakili aliyekuwa akimtuhumu kushiriki kumdhulumu.

Mama huyo, Swabaha Mohamed (Shosi), aliangua kilio mbele ya JPM, kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, Februari 2, akimtuhumu wakili Alfred Akaro wa Tanga kwa kula njama na kughushi wosia wa marehemu Mohamed Yusufu Shosi.

 Mbali na wakili huyo pia mama huyo aliwatuhumu watendaji wa vyombo vya utoaji haki kuwa wanamnyima haki. Mama huyo alidai pia kutishiwa maisha. 

Kutokana na madai hayo, Rais Magufuli alimwagiza aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP  Ernest Mangu  kumpa ulinzi mama huyo.

 Pia, alimwagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP),  kushughulikia matatizo yake na ikiwezekana waihamishe kesi yake ya mirathi kutoka Tanga.

Kutokana na tuhuma hizo dhidi ya Wakili Akaro, wakili huyo na mwenzake Abubakari Shaaban, ambaye ni mfanyakazi wa  familia ya marehemu Shosi walifunguliwa kesi ya jinai katika Mahakama ya Wilaya ya Tanga.

Katika kesi hiyo walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kughushi wosia wa marehemu Shosi na kuuwasilisha kwa familia ya marehemu Shosi.

 Hata hivyo, katika hukumu iliyosomwa jana na hakimu Lutala aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alitupilia mbali tuhuma zilizokuwa zimetolewa na mama huyo dhidi ya wakili huyo na mwenzake
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad