Picha ya Beckham Akimbusu Binti Yake Akiwa Tanzania Yazua Gumzo Kubwa ..Wazazi Wamjia Juu..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Nguli wa soka, David Beckham ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Tanzania, amezua mjadala wa kimalezi baada ya kuweka mtandaoni picha inayomuonesha akimpa busu zito la mdomo mwanae wa kike.

Baadhi ya wazazi walielezea picha hiyo kuwa haikuwa na maadili na inashangaza kwa kuzingatia kuwa mwanae Harper ana umri wa miaka mitano tu.

“Kwa kuwa mkweli, kumbusu mwanao wa kike mdomoni kama hivi kidogo inashangaza… ndio inashangaza,” aliandika mtu mmoja.

“Ninajaribu kutohukumu lakini nashindwa, lakini nadhani kidogo inashangaza na sio sawa kuona anambusu mwanae kwenye midomo kwa kuzingatia umri wake,” aliandika mwingine.

Hata hivyo, wazazi wenye mtazamo tofauti walijitokeza kumtetea mwanasoka huyo ambaye ni baba wa watoto wanne.

“Ni picha nzuri ya upendo inayoonesha uhusiano mzuri kati yako (Beckham) na binti yako,” 
aliandika shabiki mmoja. “Achana na wenye chuki. Ni wapumbavu. Harper sio binti mdogo, ni mtoto mdogo tu na hakuna ubaya kwa hilo,” aliandika mwingine.

Hivi karibuni, Beckham alionekana akiingia Tanzania kwa ajili ya kutembelea mbuga za wanyama, akiwa na familia yake. Ujio huo ulionekana kuwa binafsi na wa kimyakimya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hivo kwa nini nyie munaingilia maisha ya watu hamjaona kitu bado ni kitu cha kawaida kweli jamna kazi hadi munakua na wakati wa discuss watu fanyeni yenu hapo hapo mulipo mangapi ya sio sawa yanaendelea hivo hamjiulizi mbona watu hawalai wakawaongelea close this chapter its discussing hee hadi karaha

    ReplyDelete

Top Post Ad