Wanafunzi Shule za Msingi Wagoma, Wafunga Barabara ya Jiji Kushinikiza Wajengewe Matuta ya Marabara..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mamia ya wanafunzi wa shule ya msingi ya St. Anne wameandamana na kufunga barabara ya Jogoo jijini Nairobi nchini Kenya, baada ya basi la abiria maarufu kama ‘Matatu’kumgonga na mtu aliyekuwa akiwasaidia kuvuka barabara.

Kwa mujibu wa Daily Nation, wanafunzi hao wamefunga barabara kuu katika mji mkuu wa nchi hiyo ikiwa pia ni siku chache baada ya kuripotiwa kuwa gari moja lilimgonga na kumuua mwanafunzi mwenzao na kisha kutokomea.

Imeelezwa kuwa wanafunzi hao wameweka mgomo kwa kulala na kukaa barabarani huku wakiweka mawe katika maeneo mengine ya barabara hiyo, wakidai kuwekwa matuta barabarani hapo. 

“Tunataka haki itendeke kwa mwenzetu, hakuna matuta hakuna kusoma,” wanasikika wanafunzi hao.

Mashuhuda wa tukio la ajali wameeleza kuwa gari hilo lilikuwa likijaribu kulipita kwa kasi gari lingine kabla ya kumgonga mtu huyo aliyekuwa anajitolea kuwavusha wanafunzi.

Vyombo vya usalama vimeingilia tukio hilo na kuahidi kufanyia kazi maombi ya wanafunzi hao, baada ya magari mengi kulazimika kurudi yalipotoka kwa muda mrefu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad