Magdalena Sakaya wa CUF ya Lipumba Amwamshia Dude Maalim Seif...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya, amesema kuwa maamuzi ya kukurupuka yanayofanywa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad yanaonyesha ni namna gani kiongozi huyo anavyopungukiwa na uwezo wa kufikiri.

Amesema kuwa, Maalim Seif kwa sasa hajielewi kwani CUF inaendeshwa kwa kufuata misingi ya Katiba ya chama hicho si kama Maalim anavyofikiria kukiongoza chama hicho cha upinzani.

Ameyasema hayo mara baada ya kikao kinachodaiwa kuwa cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho kilichofanyika mjini Unguja na kuwafukuza wanachama saba wa chama hicho akiwemo Sakaya.

“Naona sasa uwezo wa kufikiri wa Maalim Seif unazidi kupungua, sijui sasa anafukuza watu kwa mara ya ngapi, hajui anachokifanya kwa sasa, kila siku amekuwa akikurupuka tu katika kutoa maamuzi,”amesema Sakaya.

Hata hivyo, amesema kuwa CUF ni chama kimoja chenye Mwenyekiti na Katibu mmoja huku manaibu katibu wakuu wakiwa wawili na kila maamuzi yanafanyika kwa kufuata Katiba ya chama hicho.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad