MAJI Kukatwa Dar, Pwani........

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini hapa (Dawasco) limesema kesho kutakuwa na katizo la maji kwa saa nane kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni kwa maeneo ya mkoa wa Pwani na Dar.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo leo, imeelezwa kuwa sababu ya kukata maji ni kuzima mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu ili kukamilisha mfumo wa umeme kwa mtambo mpya.

Dawasco imesema mtambo huo wa Ruvu Juu upo Mlandizi, Pwani na kuwataka wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi hicho.

Taarifa hiyo iliyataja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni Mlandizi Mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misugusugu, Tanita, Kibondeni, Kwa Mathias, Nyumbu na Picha ya Ndege.

Mengine ni Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba njia panda shule ya Kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba Hospitali, Kwa Mkinga, Luguruni, Kimara, Ubungo na baadhi ya maeneo ya Tabata.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad