MTU Aliyeshambulia Nyumbani Mwa Naibu wa Rais Kenya Auwawa na Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi nchini Kenya wamemuuwa kwa kumpiga risasi mshambuliaji ambaye aliingia kwa nguvu makoa ya naibu wa rais nchini Kenya Willliam Ruto.

Bwana Ruto na familia yaka hawakuwa nyumbani humo katika kijiji kilicho karibu na mji wa Eldoret.

Mwanamume huyo aliingia nyumbani kwa naibu rais baada ya kumjeruhi mlinzi wa mlango kwa upanga na kumnyanganya bunduki ayke, kwa mujibu wa polisi.

Kisa hicho kinatokea siku chache kabla ya Kenya kuandaa uchaguzi wa Rais.

Mkuu wa polisi Joseph Boinet aliviambia vyombo vya habari kuwa hali sasa imedhibitiwa.
"Hakuna tisho sasa kwa sababu alikuwa ndiye peke yake"
Hakuna taafa zaidi iliyotolewa kuhusu shambulia hilo.

Ripoti za awali zilisema kuwa watu kadhaa waliokuwa wamejihami waliingi nyumbani mwa Ruto lakini badaye polisi wakasema kuwa alikuwa ni mshambuliaji mmoja tu.

Kumekuwa na ripoti za kukamnganya kuhusu ni bunduki ngapi mtu hiyo alitumia.

Bwana Boinet aliiambia radio moja kuwa ni bunduki moja iliyokuwa ya mlinzi na imepatikana kutoka kwa mshambuliaji huyo.

Hata hivyo kamishina eneo la Ponde la Ufa Wanyama Musiambo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mshambuliaji alitumia bunduki kadha baada ya kuvunja na kuingia ghala la polisi lililo ndani ya makao hayo ya naibu Rais.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad