TUHUMA za Pole Pole Kuwanunua Viongozi wa Chadema, Mwenyewe Adai Bado Orodha ni Ndefu Kwa Wanaotaka Kuhamia CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole amesema anayo orodha ndefu ya viongozi wa upinzani wanaotaka kuhamia CCM.

Polepole amesema hayo leo huku akibainisha kuwa orodha hiyo inahusisha wenyeviti, madiwani na wabunge lakini siku nyingi tu alikuwa amewakatalia kuwapokea.

Hata hivyo Polepole amesema kwamba kutokana na kutuhumiwa kuwanunua sasa anafanya kweli, atawachukua mmoja mmoja.

Polepole amesema amemua kuchukua uamuzi huo baada ya Chadema kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kudai kuwa madiwani wanaokihama chama hicho wamehongwa na CCM.

“Sasa tutaanza kumchomoa mmoja baada ya mwingine na kwa kutekeleza hilo wiki hii watampokea kiongozi mkubwa wa chama hicho,’’anasema Polepole.

Amebainisha kuwa kama chama kinakuwa na viongozi wanaoweza kuhongwa na wakahongeka basi  chama hicho kitakuwa ni cha hovyo
"Madiwani wamesema wanamuunga mkono John Magufuli, wametoka wenyewe wameanza kusema CCM imewanunua, sasa kwa vile wameanza utovu wa nidhamu nitaanza kumtoa mmoja baada ya mwingine,’’anasema.

Polepople anaongeza kwamba: “Nilikua nakataa kuwapokea ila nina orodha kubwa wapo wenyeviti, wabunge kibao kama vile watu wanaojisaliji kodi ya majengo TRA," amesema.

"Unajua wanasema wanaisoma namba, nawahakikishia baada ya miaka mitano kwa spidi hii iliyoanza nayo CCM namba inayoonekana wakati huu itakuwa haisomeki kabisa, nitafanya shoo ndogo tu kuwachomoa viongozi hao sipendi kwenda kuwachukua wengi sababu nitaonekana kama nawahujumu vile na pia ili upinzani usikose watu angalau wa kuzungumza nao,"amesema
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Majuikana kununua ufisadi, kununua kura, kununua watu kusudi katiba isitambulike, kununua wtu wenyeakili fupi kugombea makinikia kuachia dhahabu yenyewe, kununua watu wanaotetea na kumuunga raisi asiendelee kumsomesha kijana mdogo wa kike milele hata ukijua ubovu ni elimu kwa vijana hawa na mazingira magumu lakini bado wanaunga mkono. Inashangaza watu wangapi wapo narrow minded people. Ni wengi.preaching of unrelistics. Na wengi hawaelewi.

    ReplyDelete

Top Post Ad