Wabunge Wawapongeza Watoto wa Kikwete, Nkamia Kwa Kuletea Heshima Taifa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanafunzi watatu walioshinda tuzo ya Genius Olympiad huko Marekani wametambulishwa bungeni jana kwa kuliletea Taifa heshima.

Wanafunzi hao kutoka Sekondari ya Wavulana ya Feza jijini Dar es Salaam waliambatana na walimu wao wawili. Walikuja bungeni kwa mwaliko wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwatambulisha wageni watano wa Profesa Ndalichako wakiwamo walimu wawili na wanafunzi watatu walioshinda medali za dhahabu katika mashindano ya kimataifa ya mazingira na sayansi yaliyofanyika.

“Tunawapongeza kwa kushinda tuzo hizo. Mmepeperusha bendera ya Tanzania vizuri sana,” alisema Ndugai.

Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Abdallah Rubeya, Abdularazak Juma Nkamia ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia na Khalifan Jakaya Kikwete, mtoto wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Hakusita kutania na kuwapongeza wazazi wa watoto hao kwa kusema: “Kutoka Chemba mpaka Marekani na kufanya mambo kule, kumbe inawezekana haya mambo. Lakini, hongera sana kwa Mama Salma Kikwete kwa sababu yupo Khalfan Jakaya Kikwete.”

Kukaribishwa kwao bungeni ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao ili kuwaongezea morali na kuwahamasisha wengine waliopo kwenye ngazi tofauti shuleni na vyuoni pia.

Hivi karibuni, watoto hao walipokelewa kishujaa na ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kabla hawajaletwa bungeni jana.

Walioongozana na wanafunzi hao ni mkurugenzi pamoja na mkuu wa shule hiyo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Watoto wa maskini hawana uwezo wa kujipatia elimu ya namna hii. Tujiulize, kwa nini ni watoto wa wakuu tu. Usawa, bila upendeleo.Tukitimiza hili, kunawatoto wengi wa maskini kwao hii ni ndoto. Hutaona nchi nyingi kwa watoto wa maraisi kukwezwa namna hii hadharani. Wananchi watasema moja kwa moja bila woga kuwa ni upendeleo wa hali ya juu. privilage. Cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu kwa manufaa binafsi. Na wengi wenye busara hawangeruhusu hii hadharani wakijua Watoto wetu wa kike wanaopachikwa mimba na wanasiasa, wafanya biashara, ndugu na jamaa zao, hasa kwenye maeneo tete Tanzania ambao makabila yanaruhusu mambo haya. Tujiulize kama Watanzania kwa hili.Kuwatunukia wachache, na kuwadhsrslisha maskini, na wanawake kwa ujumla.

    ReplyDelete

Top Post Ad