Dar es Salaam Yaongoza Kwa Mauaji ya Wananchi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ripoti ya nusu mwaka na Haki za Binadamu iliyozinduliwa Jumatatu Julai 31, 2017 na Kituo cha Sheria na Haki Binadamu (LHRC) inaonyesha bado hali si nzuri nchini.

Akizindua ripoti hivyo jijini dar es Salaam, Mkurugenzi wa LHRC, Dk Heleni Kijo-Bisimba amesema inaonyesha kuna ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi kutokana na watu wengi kuuawa kwa sababu mbalimbali.
Amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni, watu kadhaa wameuawa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo tuhuma za ushirikina na watu kujichukulia sheria mkononi.

“Watu 115 wameuawa wakituhumiwa ni washirikina, kati ya vifo hivyo 23 vimetokea mkoani Tabora ambao unaongoza, ukifuatiwa na  Kigoma wenye vifo 23 na Kagera vifo 11,” amesema Dk Kijo-Bisimba.

Amesema matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi nayo yamerudi kwa kasi kwani taarifa za Polisi zinaonyesha kuwa watu 479 wameuawa na wananchi wenye hasira.

Mkoa wa Dar es salaam ndiyo unaongoza kwa matukio hayo kwa kuwa na vifo 117, ukifuatiwa na Mbeya vifo 33, Mara 28 na Geita 26.

“Taarifa ya kipindi hiki inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za raia hususani haki ya kuishi, lakini pia ukiukwaji mkubwa wa haki za makundi maalum hasa wanawake na watoto,” amesema.
Amesema pia kuna vifo tisa ambavyo vinahusisha vyombo vya dola, ingawa Jeshi la Polisi katika taarifa yake inaonyesha ni mtu mmoja pekee ndiye aliuawa akiwa mikononi mwao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad