Hatimaye Hali ya Mbunge wa Bunda Ester Bulaya Yaendelea Kuhimarika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye Hali ya Mbunge wa Bunda Ester Bulaya Yaendelea Kuhimarika
Hali ya Mbunge wa Bunda Ester Bulaya aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH ) inaendelea vizuri baada ya kuanza kupatiwa matibabu jana.

Bulaya ambaye alipata tatizo la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya Kituo cha Kati cha Polisi mjini Tarime, alifikishwa hospitalini hapo juzi usiku na kulazwa katika wodi namba 18 Sewahaji.

Akizungumza Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Stephen alisema leo Bulaya amepata ahueni kiafya na anaendelea vizuri na matibabu.

"Sasa ameanza kujihudumia mwenyewe, anakula vizuri na bado anaendelea na matibabu," amesema Stephen huku akisisitiza kuwa mgonjwa bado anahitaji utulivu kwa kipindi hiki.

Bulaya amesota rumande tangu akamatwe Ijumaa ya Agosti 18 kwa madai ya kuingia jimbo la Tarime na kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi jimboni humo baada ya kualikwa na mbunge mwenzake Ester Matiko.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad