Israel: Iran Inajenga Kiwanda cha Makombora Syria

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Israel: Iran Inajenga Kiwanda cha Makombora Syria
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inajenga viwanda nchini Syria na Lebanon ili kutengeza makombora.

Benjamin Netanyahu ameishutumu Iran kwa kuifanya Syria kuwa kambi yake kutengeza vifaa vya kijeshi kama mpango wake wa kutaka kuiangamiza Israel.
Majeshi ya Iran yanamsaidia rais Bashar al Assad katika vita vya Syria huku ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Lebanon Hezbollah.

Matamshi ya Netanyahu yanajiri baada ya kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutierrez mjini Jerusalem
Bwana Guterres amefanya ziara yake ya kwanza katika enewo hilo tangu kuchukua mamlaka mnamo mwezi januari.

Bwana Netanyahu hakutoa maelezo kuhusu viwanda hivyo vya Iran lakini akaonya kwamba hicho ''ni kitendo ambacho Israel haitakubali''.
Wiki mbili zilizopita, kampuni ya Israel Imgesat ilichapisha picha ilizosema zinathibitisha ripoti ya gazeti moja la upinzani nchini Syria kwamba kiwanda cha makombora kilikuwa kikijengwa kaskazini magharibi mwa Syria chini ya uangalizi wa Iran.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad