KASSIM MGANGA : Natumbuiza Kwenye Harusi kwa Tsh. Milioni 5

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KASSIM MGANGA : Natumbuiza Kwenye Harusi kwa Tsh. Milioni 5
Msanii wa Bongo Flava, Kassim Mganga arigia kiasi cha fedha anachokipata kutokana na kutumbuiza kwenye harusi ukilinganisha na show za kawaida.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kitendawili’ aliyoshirikishwa na Mrisho Mpoto, ameiambia FNL ya EATV kuwa harusi moja huweza kumuingizia Tsh. Milioni 5 na anafanya hivyo kutokana kwa sasa ana band.

“Arts kama arts unatakiwa ufanye kazi na kazi zina mazingira mengi sana, mimi ninafanya vitu vingi sana, nimeanza game tangu 2005 mpaka leo. Sasa hivi nina band natumbuiza kwenye harusi kwa milioni tano,” amesema.

“Sasa thamani ya arts ambaye anatumbuiza kwenye harusi kwa kiasi cha milioni tano na arts ambaye anakwenda Morogoro kila kukicha kwa milioni moja hapo vipi?,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Kassim amekanusha taarifa kuwa yeye kujikita zaidi katika harusi kunashusha muziki wake kwa kueleza msanii anatakiwa kufanya vitu vingi.

Utakumbuka kipindi Belle 9 na G Nako wanatoa wimbo wao ‘Ma-Ole’walitangaza kuanza kazi ya kutumbuiza kwenye harusi kupitia ngoma hiyo na iwapo mteja atahitaji zaidi wapo tayari kumtungia wimbo mwingine.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad