Kimenuka Mgodi wa Acacia Wananchi Waandamana Kushinikiza Malipo Yao.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kimenuka Mgodi wa Acacia Wananchi Waandamana  Kushinikiza Malipo Yao.
Wananchi wanaoudai mgodi wa Acacia North Mara fidia ya maeneo yao kwa kukaa muda mrefu bila kuwalipa, wameandamana kwenda mgodini kushinikiza malipo yao.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe amesema maandamano hayo yanafanyika mara kwa mara kutokana na baadhi ya  majina kuondolewa kwenye orodha ya waliohakikiwa.

Kamanda Mwaibambe amesema kuwa majina ya watu hao yaliondolewa kwenye orodha hiyo na mgodi huo baada ya kukutwa yameongezeka wakati wa kuwasilishwa mgodi hapo kwa malipo yaliyotakiwa kutolewa na kufanya shughuli ya ufidiaji kukwama.

Hata hivyo, kundi hilo la wananchi limetawanywa na polisi waliokuwa na gari la maji ya kuwasha ambalo limesimama kwenye lango mkuu la kuingia mgodi .

"Nina taarifa ya kuwepo kwa maandamano hayo siku za nyuma, lakini kwa siku ya Leo sina hiyo taarifa labda nifuatilie utanicheki baadaye," amesema Kamanda Mwaibambe.

Ameongeza kuwa baada ya mgodi huo kubaina kuwepo kwa ongezeko la idadi ya wanaodai wafidiwe maeneo yao, waliandika barua kwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga ili kulishughukikia.

"Mkuu wa wilaya ndiye anayeweza kulisemea hilo vizuri maana nijuaavyo mimi alikabidhiwa orodha hiyo kwa ajili ya kuishughulikia," amesema.

Hata hivyo, simu ya mkononi ya Mkuu wa Wilaya, Luoga ilipopigwa kujua hatua iliyofikiwa kwa wananchi hao kupata haki yao, haikuwa hewani.

Hivi karibuni kundi la wananchi lilivamia kwa siku mbili mfululizo mgodi huo likitaka kuokota mawe ya dhahabu ambapo watu zaidi ya 60 walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uvamizi na hadi sasa wapo rumande.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad