Kimenuka..Emmanuel Mbasha Amvua Nguo Madam Flora Mbasha.....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BAADA ya mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bongo, Flora Mbasha kusambaza kitabu alichokipa jina la Siri za Flora Mbasha kilichoanika ‘mabaya’ ya aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha, mumewe huyo ameibuka na ‘kumchana’ vibaya mwimbaji huyo na kusema hafai kuwa mke.

Flora alikiachia kitabu hicho hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine aliyopitia kwenye maisha yake na Mbasha, alieleza namna ambavyo mumewe huyo wa zamani alivyokuwa akimtesa na hata kumuingilia kwa nguvu akiwa kwenye siku zake.
Akizungumza na mwanahabari wetu katika ofisi za gazeti hili, Bamaga- Mwenge jijini Dar, Mbasha alianza kwa kueleza masikitiko yake juu ya kitabu hicho kwa kusema anashindwa kuelewa mume wa sasa wa Flora, Daud Kusekwa anajisikiaje pale Flora anapomzungumzia mara kwa mara.
“Yaani unajua watu wengine sijui wapoje bwana. Hivi kweli wewe hata huyo mwanaume wake anajisikiaje kuona mkewe ananiongelea kila wakati? Ni kukosa adabu, kwa nini wasifanye maisha yao?


“Kweli mwanamke aliyefunzwa, akafunzika anaanzaje kumuongelea mwanaume wake wa zamani? Yaani kwangu mimi mwanamke wa aina hiyo anapoteza sifa ya kuwa mke,” alisema Mbasha.
Mbasha akizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Amani, alisema kuwa, aliamua kukaa kimya baada ya kupitia mambo mazito na mwanamuziki huyo ambayo kamwe hataki kuyasikia wala kurudi nyuma.
“Ametaka talaka mahakamani, tumeachana na mimi sikutaka tena hata kumzungumzia, lakini yeye kutwa amekuwa akinizungumzia. Halafu kwanza unamzungumziaje mtu ambaye mlishaachana? Mtu ambaye kwanza hana hata habari na wewe, anafanya maisha yake mengine, huu kama siyo ujinga ni nini?” Alihoji Mbasha.

Kama hiyo haitoshi, Mbasha alizidi kumwaga mboga kwa kusema kuwa, siku zote sikio la kufa huwa halisikii dawa kwani kitendo anachokifanya Flora cha kumzungumzia yeye kama zilipendwa wake, alishakifanya kwake kwa mwanaume mwingine.
“Kifupi ni kwamba tabia ni kama ngozi, huwezi kuibadili. Wewe unaona sasa hivi anavyoelezea mambo aliyokuwa akiyafanya na mimi na kuongeza uongo wake, alishanifanyia hata mimi wakati nimemuoa.

“Yaani yule mwanamke sijui bana, Mungu amsaidie. Yaani kwanza wakati mimi naanza kumfuatilia, huwezi kuamini, alikuwa na mwanaume mwingine. Akamuacha kwenye mataa wakati tayari walikuwa wanaelekea kwenye ndoa na vikao tayari walikuwa wameshaanza kufanya,” alisema Mbasha.
Mbasha ambaye kwa sasa hajaingia kwenye ndoa tangu aachane na Flora, alisema kuwa, anamshauri Flora aache kumzungumzia kwani kama ni ndoa ilishavunjika, aitazame zaidi ndoa yake mpya.

“Aachane na mimi. Namshauri atulie kwenye ndoa yake kuliko kila kukicha ni Mbasha… Mbasha…,” alisema Mbasha.
Mbasha na Flora walidumu kwenye ndoa kwa miaka 12 na kubarikiwa mtoto mmoja kabla ya kuachana mahakamani.
Kabla ya kuachana huko, Mbasha alituhumiwa kumbaka mdogo wa Flora na kesi kuunguruma muda mrefu na baadaye Mbasha alishinda hivyo kuachiwa huru.

 STORI: ERICK EVARIST | GAZETI LA AMANI
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mjinga huyo.. hata ya mume wake huyo mpya atayaanika tu, she is very sick in the head.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sasa ujiga wake nini leba sikaingia mwenyewe

      Delete
  2. ukiona hivyo bado anampenda

    ReplyDelete
    Replies
    1. kabisa...!!!! wanawake wote walivyojaa.. huoni ila Flora .. flora mwenzako bado anakumindi.. hembu mlani shetani mrudiane... mungu baba atashuhudia hilo..mbashe punguza usongo ..Flora atarudi tu. anza hata vimedeji meseji vya wasup. unayo smatiphone?? itabidi ujismatiphonishe ili flora akutag..halafu una hashtag## Flora rudi.

      Delete

Top Post Ad